Mwaka mpya wa fedha 2011/12 vs bei za mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka mpya wa fedha 2011/12 vs bei za mafuta

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Njowepo, Jul 3, 2011.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Leo ni tarehe 3 siajaona mabadiliko ya bei maeneo mengi mfano Mbeya Diesel bado ni 2300 na iringa 2100.
  Ivi ewura walikuwa wanatania?
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  inashangaza kweli, badala ya kushuka ndo inapanda, lakini nikuulize....hiyo bei uliyoweka ni kwa ujazo gani?
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sorry ni 2100 kwa 2300 kwa lita si unajua izi keyboard za mahadhi ya kifaransa zasumbua
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  [h=2]Ewura: Msihofu bei ya mafuta taa haitapanda[/h]
  Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Maji (Ewura)
  Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Maji (Ewura), imewatoa hofu wananchi kuwa bei ya mafuta ya taa haitapanda kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakihofia.
  Hayo yalisemwa jana na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Titus Kaguo, kwenye Maonyesho ya Sabasaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, jijini Dar es Salaam.
  Alisema baada ya serikali kutangaza kuwa imeongeza kodi ya mafuta ya taa kwa Sh. 400, wananchi wengi wamepata hofu kuwa bei ya bidhaa hiyo itapanda kwa kiasi hicho.
  "Si kweli kwamba bei ya mafuta ya taa itapanda kwa Sh. 400, hiyo ni kodi kwa mwagizaji wa mafuta ambaye awali alikuwa akilipa kodi ya Sh. 52 kwa lita," alifafanua Kaguo.
  Alieleza kuwa, punguzo la tozo ya Sh. 224 limetolewa na serikali kabla ya bidhaa hiyo kumfikia mlaji, hali ambayo inaondoa uwezekano wa bidhaa hiyo kupanda bei.
  Alisema baada ya punguzo la tozo hiyo, bei kwa mlaji inaweza kupanda kwa Sh. 123 tu na kwamba shughuli ya ukokotoaji wa bei ya bidhaa mbalimbali bado inaendelea.
  "Shilingi 123 ni bei ambayo huwa tunaionyesha kwenye matangazo ya bei elekezi kwa mafuta ya taa, hivyo katika kuongeza kodi mlaji hajaumizwa kama watu walivyodhani," alisema Kaguo.
  Meneja Mawasiliano huyo wa Ewura, alisema lengo la kupandisha kodi ya mafuta ni kumaliza tatizo la uchakachuaji na wala si kumkomoa mlaji wa mwisho kama watu walivyodhani.
  Alisema awali wafanyabiashara wasio waaminifu walikuwa wakiagiza mafuta ya taa kwa wingi na kuyachanganya na dizeli, lakini kwa punguzo la sasa hawawezi kufanya hivyo.
  "Tofauti ya kodi ilikuwa kubwa sana na iliwashawishi wafanyabiashara kuagiza mafuta ya taa kwa wingi na kuchakachua, lakini hivi sasa tofauti ni ndogo sana na haiwezi tena kuwashawishika kufanya mchezo huo mchafu," alisema Kaguo.
  Kabla ya mabadiliko hayo, kodi ya dizeli ilikuwa Sh. 514 na ile ya mafuta ya taa ilikuwa Sh. 52 kwa lita, hali iliyowafanya wafanyabaishara kuagiza mafuta ya taa kwa wingi na kuyachanganya na dizeli ili kupata faida kubwa.
   
Loading...