MWAKA 2023: Mwaka wa Tafakuri na Katika Mpya - 2

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Mwalimu Julius Nyerere alisema kuwa mpinzani wa kweli ni lazima atokee ndani ya CCM, Je maono ya Mwalimu yalimlenga Hayati Rais John Pombe Magufuli, kwa namna anavyochukuliwa sasa hivi ndani ya CCM,ni kama alikuwa mpinzani ndani ya CCM. Au je kauli ya Mwalimu ilimlenga Ndugu Edward Lowassa baada ya kung'atuka CCM na kwenda Chadema au tungoje kauli ya Mwalimu Nyerere ipate kutimia!?

Nauona mtifuano ndani ya chama kikubwa katika Mwaka 2023 utafanya wazee wenye mvi kufanya maamuzi magumu kunusuru chama ni maamuzi gani na nini kitatokea!? muda ni mwalimu,kutokana na safisha safisha ya serikali ndani ya serikali ajira zitakuwa nyingi kuziba mianya ya walio ondolewa kwa uzembe na Mambo mengine.

Mwaka huu 2023 kutokana na ugumu wa maisha watu watahoji ilikuwaje hadi wakatokea watu wakatuibia mamilioni ya fedha kupitia ununuzi wa rada? Wakatuleta mikataba ya kiajabu ajabu kama ya Richmond na Escrow,Ilikuwaje wakaja jamaa na kampuni yao ya magirini wakituahidi kuwa watatatua tatizo letu la umeme? Wengine watasema tuwe na kipengele cha "power of Recall".

Mwanachi asiwe na nguvu tu wakati wa uchaguzi ila kama kiongozi anafanya vibaya Wananchi wawe na uwezo wa kumuwajibisha hata kabla ya miaka mitano,Mimi hoja yangu siku zote ni kuandikwa katiba mpya wala sio kubadilisha.

Sababu za kuandika katiba mpya ni nyingi, lakini ya msingi kabisa ni kuwa wananchi wa Tanzania hawajawahi kushiriki katika kupambanua mambo wanayotaka yawe kwenye katiba yao,rasimu ya Jaji Warioba iliwafikia baadhi lakini wanasubiri hadi mambo yawakute,kwa hiyo ni wazi kabisa katiba uhalali wa katiba yetu hasa katika mazingira ya leo ni jambo lenye kuzua maswali mengi kuliko majibu.

Baadhi ya mambo ninayoshauri kuandikwa kwenye katiba mpya ni kama ifuatavyo:

(1) Rais asiteue mawaziri ma RC, DC na mabalozi kutokana na wabunge. In fact mad-DC, na ma-RC wasiteuliwe, hawa wachaguliwe na wanachi kusudi kuwafany wawe more accountable kwa wananchi.

(2) Rais asiteuwe wabunge wake wenyewe.

(3) Uteuzi wa Mawaziri majaji, makamanda wa polisi, na makamanda wakuu wa majeshi ukamilishwe na Bunge, Rais atoe pendekezo na bunge ndilo likamilishe uteuzi. Baada ya kupitisha na Bunge, Rais asiwe na madaraka ya kuwafukuza kirahisi bila bila kupata baraka za Bunge.

(4) Bunge liwe na uwezo wa kumvua Rais na viongozi wengine madaraka yao ikithibita kuwa utendaji wao haukufuata maadili ya madaraka hayo.

(5) Kuundwe tume ya utumishi wa serkali inayojitegemea; uteuzi wa tume hiyo ufuate utaratibu sawa na (2) hapo. Tume hii iwe na wajibu wa kuhakikisha kuwa wafanya kazi wa serikali hawaingizi siasa katika shughuli za serikali.

(6) Tume ya uchaguzi iwe huru; iundwe kwa kufuata utaratibu wa (2) hapo juu.

(7) Muundo wa serikali uandikwe kwenye katiba, yaani wizara na idara za serikali zijulikane kikatiba, siyo Rais akurupuke na kuunda baraza la mawaziri 100 ili kuridhisha marafiki zake.

(8) Viongozi wa serikali wasiwe na madaraka ya kutoa vyeo au kufukuza wafanya kazi wa serikali; shughuli hiyo iachiwe tume ya utumishi kwa wafanya kazi wa ngazi ya kati na ngazi ya chini, na bunge liwe na madaraka juu ya wafanykazi wa ngazi za juu kama vile makamishna wa idara na makatibu wakuu wa wizara kwa kushauriana na tume ya utumishi. Viongozi wa serikali wanaweza kupendekeza tu.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on poverty reduction.
 
Back
Top Bottom