Mwaka 2020 ni wa maamuzi magumu kwa jimbo la Kawe

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Mtandaoni kuna kipande cha maongezi kinachosambazwa kati ya mbunge wa Kawe na watu wawili tofauti.

Wananchi hao ambao nadhani ni wakazi wa jimbo la Kawe wameshindwa kumtunzia heshima Dada Halima Dede ni kuonyesha ni kwa jinsi gani walivyokerwa na tabia yake ya kugombana mara kwa mara na mamlaka za Bunge.

Wakati mwingine kwa mtu mwenye kupima masuala kwenye mizania sahihi ipo haja ya kumpa faida ya mashaka (benefit of doubt) mbunge Halima Mdee, kwa kuamini kuwa mheshimiwa Spika au Naibu wake hushindwa kutawala mijadala na huzidiwa nguvu na mihemko ya vikao na hivyo hutoa maamuzi yasiyo na upendeleo kwa mbunge.

Lakini baada ya kuyaona hayo maongezi kati ya Mbunge Halima (nasita kuamini kwamba ni fake) na wananchi walioamua kumtusi mtandaoni, ninadhani Dada Halima analo tatizo la personality.

Unapokuwa mwakilishi wa wananchi, hupaswi tena kuwakwaza moja kwa moja hata kama unadhani upande wake upo sahihi. Sasa kwa utovu wa adabu wa dada huyu nadhani wapiga kura wa Kawe wanayo kila sababu ya kufanya maamuzi magumu mwaka 2020.

Jimbo la Kawe ni mojawapo wa majimbo yenye ushawishi mkubwa Tanzania. Viongozi wengi nchini, aidha wanaishi katika jimbo hili au wanamiliki viwanja, hivyo ni wakazi wa Kawe.

Ni jimbo ambalo linahitaji mbunge mwenye kitu kipya chenye kulingana na aina ya matarajio ya watu wengi wenye kujiheshimu na kutambua maana ya heshima.

Kama wewe ni mkazi wa Kawe, basi 2020 fanya uamuzi mgumu kwa lengo la kuirudisha heshima ya sehemu unayoishi.
 

Attachments

  • IMG-20170607-WA0035.jpg
    IMG-20170607-WA0035.jpg
    33.4 KB · Views: 64
Halima anatetea wananchi wa jimbo lake na watanzania kwa ujumla, Sema 2020 watanzania tufanye maamuzi sahihi kwa yule anayetutukana mara kwa mara kwenye majanga na misiba, mara hakuna chakula cha bure, mara tetemeko halikuletwa na ccm n.k.
 
Ni mtu mjinga pekeyake ndio atasapote hu upumbavu so kwa watu wajimbo lakawe ni vichwa safi kuliko chakwako kwanza hawaishi kwa propaganda za kijinga wanajua nini wanakifanya
Mkuu wewe hukai jimbo la Kawe, wewe ni wale tunawaita bendera hufuata upepo. Nyinyi ndio mnaodeki barabara wakati wa kampeni.

Nalisikitia jimbo la Kawe kwa sababu linanihusu, nahisi aina fulani ya ukakasi kila nikiona kituko baada ya kituko cha huyu dada.
 
Back
Top Bottom