Mwaka 2020 kutakuwa hakuna tembo Tanzania

Mwaka 2020 kutakuwa hakuna tembo Tanzania

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Leo katika mkutano wa siku mbili unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, wanamazingira wamedai kuwa ujangili unatisha sana kiasi kwamba kufikia mwaka 2020 kutakuwa hakuna tena tembo Tanzania. Wanadai kuwa karibu tembo 30 wanauawa kila siku hapa nchini. Akifungua mkutano huo mapema hivi leo, Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal, amesema kuwa mwaka 2006 Selous-Mikumi ilikuwa na tembo 70,000 lakini mwaka jana ilikuwa imebakiwa na tembo 13,000 tuu.

Wakati huo huo leo majira ya asubuhi Cambodia wamekamata kontena lenye zaidi ya tani tatu za pembe za ndovu (Cambodia seizes three tonnes of ivory). Maafisa wa nchi hiyo wamesema pembe hizo zilikuwa zimehifadhiwa ndani mifuko 108 na kufichwa kwenye kontena lililokuwa na maharage. Wamesema kontena hilo liliingizwa nchini humo kutoka nchi nyingine lakini wamekataa kuitaja hiyo nchi.

Taarifa za chini chini kutoka vyombo vya habari vya Cambodia zinadai kuwa kontena hilo lilitokea Malyasia lakini bado haijulikani lilisafirishwa kutoka nchi gani na kuingia Malaysia kabla ya kupelekwa Cambodia. Inasemekama lilikuwa lipite Cambodia kelekea nchini nyingine. Kwa mujibu wa World Wildlife Fund, kilo moja ya pembe inauzwa zaidi ya dola za Kimarekani 2,200.

========================

Poaching could wipe out Tanzanian elephants in 7 years: Conservationists

Poachers are slaughtering Tanzania's elephants for their ivory at such alarming rates that the population could be completely wiped out in just seven years, conservationists told a conference on Friday.

The two-day UN-backed conference which opened on Friday aims to come up with strategies to stem worsening elephant poaching in Tanzania, a top safari destination determined to protect its prized wildlife assets but struggling to deal with increasingly sophisticated organised crime gangs.

"Approximately 30 elephants a day are killed... at this rate the population will be exterminated by 2020," the Tanzanian Elephant Protection Society (TEPS), an independent conservation group, said.

Tanzanian Vice President Mohamed Gharib Bilal opened the summit by asking for international assistance in battling the increasingly well-organised and equipped poaching gangs. "Organised and intricate poaching networks in and outside the country sustain this illegal trade, thus making it difficult for Tanzania alone to win this battle," Bilal said, painting a bleak picture of the situation.

Source: Poaching could wipe out Tanzanian elephants in 7 years: group
 
Inawezekana kabisa, licha ya mashirika mbalimbali kuonya kuwa Tembo watatoweka bado mtasikia bajeti ya wizara husika haijatenga fungu la kupambana na majangili wa Tembo. Tunataka kupambana kwa "msaada wa watu wa marekani". Mi nasubiri bajeti nione then nifanye conclusion kuwa Tembo watatoweka au lah!
 
4 SURE THE SITUATION IS TERRIBLE. R.I.P LOXODONTs
 
Hurumaaa....masikini mwanangu hatoziona tembo
 
Hurumaaa....masikini mwanangu hatoziona tembo

Haya yote ni kile chama na katibu wake ndo watafanya watoto wetu waone tembo kwenye picha na sio kwenye mbuga tena
 
Ngoja tusubiri hotuba ya Nyala bungeni kasema atawataja majangili. Sijui kama atakuwa na uthubutu wa kuwataja wale wabunge waliokwishabainika walihusika!
 
Inabidi tutengeneza CD ya tembo wa Tanzania ili watakapoisha tutumie CD kuwaonesha watoto wetu.
 
Huyo vice President atakuwa ameisoma hiyo report kama hadithi tu. Hatakuwa na msaada wowote wakati boss wake ameshakiri kuwa anawajua hao wahalifu.
 
Muda si mrefu watanzania tutakuwa tunaenda kuangalia tembo na wanyama wengine Middle East.
 
Tanzania needs to address the root of the problem which is China, we need to run massive PR campaigns in Chinese media as well as other asia countries on the effects fo their ivory Consumptions.

Good thing is Chinese are very passive individuals and No Chinese Man would dare show his pride of Ivory in front of Family and Friends if its being perceived as a bad things by the society.

And this can be done by dealing with Big Chinese Influencers, like Chinese sports Legends and popular artists.

I remember YaoMing did a documentary on elephant poaching last year, we need such imagery on all chinese Subways from Beijing, Shanghai, Guangzhou, HK, Tianjin, Taipei etc.,

This has been done with regards to drug use in HK, it has been done with regards to SAR and recently to combat illegal shark fishing for shark fins.

That way they will see the ivory they value so much is nothing more than death to animals, as of now there is no real connection to Chinese people, for them, it seems like wearing diamonds,or Gold. am sure most thinks Ivory comes from the ground in African villages.

Yaoming looking at a dead Elephant without ists tusks

th



Yaoming looking at two elephants with no tusks

watchingelephants.jpeg


Images like these should flood Asian Cities particularly Chinese

6388839_1200x1000_0.jpg




imagine this image in a dongzhimen or Tsim sha Tsui stations, i can be confident its enough to reduce 30-60% of poaching without firing a single bullet. Adding that with PR campaigns in other media, it shpuld help a lot. Thats my two cents, Maliasili kazi kwenu, sio kuja kuuza nyaga tu kila mwaka ughaibuni wakati wanyama wanaisha.


Yao-called-seeing-a-dead-poached-elephant-a-sight-I-will-not-soon-forget.-AP.jpg
 
hivi kweli mpaka mtu aende hifadhi akapige tembo tena kwa bunduki na mrio wake magemu wasisikie?hebu tusidanganyane biasha hizi halamu hazifanywi na masikini zinafanya na matajiri,maana kama kilo moja ya pembe ni 80elfu mpaka laki,na uuzwaji wake mkubwa ni burundi na huko ugaibuni huyo masikini ambaye hata pasport hana atakwendaje na ataludije,siku zote mkubwa akipumua akawepo mtoto,mtoto ndo husingiziwa.
 
Kinana na magamba wenzako mnamaliza tembo wetu ili mpate pesa za kusomba watu na kununua viongozi wa chadema na vyama pinzani kwa ujumla...

Kikwete janga la taifa
 
hadi hili limewashinda... uraia nchi nyingine fasta sio kuishi na wapuuzi
 
hivi kweli mpaka mtu aende hifadhi akapige tembo tena kwa bunduki na mrio wake magemu wasisikie?hebu tusidanganyane biasha hizi halamu hazifanywi na masikini zinafanya na matajiri,maana kama kilo moja ya pembe ni 80elfu mpaka laki,na uuzwaji wake mkubwa ni burundi na huko ugaibuni huyo masikini ambaye hata pasport hana atakwendaje na ataludije,siku zote mkubwa akipumua akawepo mtoto,mtoto ndo husingiziwa.
wanashiriki sana hadi wanaazimisha silaha
 
Haya yote ni kile chama na katibu wake ndo watafanya watoto wetu waone tembo kwenye picha na sio kwenye mbuga tena

Nafikiri tusimame pamoja kama taifa tuachane na kunyooshea kidole watu. Kama wote tutakataa tutaweza kuwanusuru tembo wetu. Bali Kama tutasubiri ccm wafanye it would be too late when we wake up.
 
Kinana hongera,
kazi yako inaonekana, na imeanza kutambulika kimataifa
 
Back
Top Bottom