Mwaka 2011 unaisha: Je Umefanya nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka 2011 unaisha: Je Umefanya nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elli, Dec 13, 2011.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Wapendwa, mwaka 2011 umekuwa na changamoto zake nyingi tu; Je umejenga utamadauni wa kujitathmini? Je yale uliyoyataka yametimia kwa kiasi gani? Je mipango yako na ndoto zako ulijitahidi kuifikia kwa kiasi gani?

  Kwangu mimi na wewe ni kipindi muhimu sana cha kumshukuru MUNGU au yeyote yule unayeona alikuwa muhimu kwa mafanikio yako ( Mimi na Nyumba yangu tutamshukuru MUNGU).


  Wapo wengi walitamani waione leo hii, wauone mwaka huu, wakapanga na mipango, wakaota na ndoto, leo hatunao, wengine wako vitandani, wengine wamefanikiwa, ni wakati wa kumuomba na kumshukuru MUNGU.

  Samehe, sahau, jitathmini pale ambapo ulishindwa usipaite TATIZO but pachukulie kama changamoto ya kukuwezesha kuvuka na kuendelea mbele zaidi, pengine lile ulilolitaka halikua, pengine ndoto yako haikutimia, badala ya kukaa na kuanza kuangalia ya nyuma (ambayo hayasaidii kwa future) angalia what you have now, angalia ni namna gani utafanikiwa zaidi kwa mwaka 2012, panga mipango sasa, ota ndoto zako zote sasa kisha jenga na weka misingi ya kuzigeuza ndoto hizo kuwa kweli.


  Tuwasemehe hata wale wanaoitakia mabaya nchi yetu, wanaotunyanyasa na kutuibia kwa wizi wa mchana kweupe, tuombe kwa ajili ya wanafunzi wote walionyimwa mikopo huku billions zikiteketea kwa one day event, tuombe kwa ajili ya watoto wetu na ndugu zetu wanaosoma chini ya miembe na mikorosho huku wakikaa chini na wengine waliojengewa mabanda yasiyo na walimu wala elimu ambapo wengi wao wameishia kuvuta babgi na binti zetu kugeuzwa bidhaa za majangili, ndio shule za kata tutanzojivunia. Tumombe hata kwa ajili ya akina Mama wajawazito wanaofariki njiani kwa kukosa huduma za afya na Ambulance huku magari ya kifahari yakinunuliwa kila siku, tuombe hata kwa ajili ya wazee wetu ambao wamedhulumiwa haki zao za kuishi na kulipwa ujira usiostahili, tuombe hata kwa ajili ya wale wanaowanywesha ndugu zetu sumu kwenye migodi huku wakilindwa kwa mitutu ya bunduki, MUNGU tuangazie wana wako ili mwaka 2012 haya yapungue.

  Nawependa sana na nawatakia Mapumziko mema ya mwisho wa mwaka, tujihadhari kwa mambo ya dunia (anasa)ili tuyafikie malengo yetu.
   
 2. MANI

  MANI Platinum Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,408
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  "Tuwasemehe hata wale wanaoitakia mabaya nchi yetu, wanaotunyanyasa na kutuibia kwa wizi wa mchana kweupe, tuombe kwa ajili ya wanafunzi wote walionyimwa mikopo huku billions zikiteketea kwa one day event, tuombe kwa ajili ya watoto wetu na ndugu zetu wanaosoma chini ya miembe na mikorosho huku wakikaa chini na wengine waliojengewa mabanda yasiyo na walimu wala elimu ambapo wengi wao wameishia kuvuta babgi na binti zetu kugeuzwa bidhaa za majangili, ndio shule za kata tutanzojivunia. Tumombe hata kwa ajili ya akina Mama wajawazito wanaofariki njiani kwa kukosa huduma za afya na Ambulance huku magari ya kifahari yakinunuliwa kila siku, tuombe hata kwa ajili ya wazee wetu ambao wamedhulumiwa haki zao za kuishi na kulipwa ujira usiostahili, tuombe hata kwa ajili ya wale wanaowanywesha ndugu zetu sumu kwenye migodi huku wakilindwa kwa mitutu ya bunduki, MUNGU tuangazie wana wako ili mwaka 2012 haya yapungue."

  Mpwa kati ya mambo yanayonikera ni hayo hapo juu! Hivi mbona wakati wa 60-70's tuliweza kusoma katika hali bora pamoja na kuwa na vyanzo vidogo vya mapato kwa serekali. Hii inaonyesha kuwa utawala wa mwanzo ulikuwa unajali watu na sio huu wa matanuzi. Mungu atasikia dua zetu Ameen !
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Wakati nafanya degree yangu ya kwanza ya education, Profesa Mushi PAK alionyesha fact moja ambayo kidogo tu ingenitoa machozi; kwamba Tanzania ndio ilikua mbele kwa literacy level kuwa ndogo kubwa( yaani watu wengi walijua kusoma na kuandika) na Mwl. Nyerere na Mama Nyerere walikuwa na madarasa yao, kulikua na maktaba kila wilaya na vitabu vilikuepo!! Leo hii Tanzania mambumbu ndio yameongezeka sana si kosa lao bali la mfumo; tuombe MUNGU mambo haya yabadilike na sisi tuendelee mbele.
   
 4. hirorobert

  hirorobert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sijaambukizwa AIDS
   
 5. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Asante
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  mmh afadhali kama huna ukimwi
   
Loading...