Rafiki yangu Porokondo wikiendi hii amenihadithia kisa kilichomkumba miaka mitatu iliyopita nami nikaona ni vyema niwawekee hapa.
Porokondo ni kijana mtanashati na japo sasa umri umesogea kidogo lakini bado uchekibobu wake wa miaka ile ya balehe haujamtoka kabisa. Sikuwahi kumuona tangu tulipopotezana yapata miaka sita sasa, basi juzi niko kwenye sehemu zetu za kupata moja baridi na moja iliyopoa pale KWA AMINA , mara hamadi namuona mtu kama namfahamu hivi.. Basi macho yalinitoka na kwa furaha na kwa sauti kuu nikaita "Porokondooooo, Porokondoooo"… Jamaa kwa uchekibobu wake akatoa mawani yake meusi na kunitazama na nashukuru sana Maulana naye alinikumbuka.
Nisiwachoshe: Basi tukaketi pale huku AMINA akituletea kama tulivyokua tukiagiza, jamaa yangu yeye kwa kuwa anapenda vitu laini laini alikua akigonga Castle Light zake taratibu, lakini mara zote macho yangu yalikua yakishangaa alama za makovu zilizoonekana katika mikono yake wakati akinyanyua chupa na kumeza mafundo!! Huyu jamaa tangu nimemfahamu hajawahi kutumia glass baa kisa anaogopa kwamba eti hazisafishwi vizuri. Sikuweza kumuuliza lolote maana tulikua hatujaonana muda mrefu na sikutaka tu kuanza kuingilia mambo yake na wasiwasi wangu nilidhani inaweza kuwa alipata ajali hivyo sikutaka kabisa kumkumbushia machungu.
Pombe hazina maana!! Wakati tunaendelea na mazungumzo huku harufu ya mishikaki ya Nundu ikisikika kutoka jikoni,Porokondo alikua anamalizia chupa yake ya Tano, akaniambia "Kaka Amani wewe unanifahamu zamani na nimekuona jinsi ulivyokua ukitazama mikono yangu, ngoja nikusimulie kilichonipata"
Akaniambia miaka mitatu iliyopita kiu ya ujana ilimshika akaamua kutembelea maeneo ya sinza nyakati za usiku ili kutafuta kipoozeo na wakati wa zunguka zunguka yake aliishia baa ya MEEDA huko mitaa ya MORI. Ilikua ni kama saa sita usiku hivi wakati amewasili pale, basi akaagiza bia yake baridi huku akiwaangalia mabinti waliokua wakijipitisha kwa deko na mashamsham ya kuashiria wako sokoni. Alipopepesa macho, hamadi! Akaona mtoto kafungashia yaani anasema kwa mfungasho ule kama angechafua hewa leo jumatatu basi harufu ingesikika Alhamisi.
Basi wakaongea pale wakakubaliana shing aafu kumi short time.Shida ikaja jamaa hakua vizuri mfukoni kuupeleka Mfungasho ule kwenye nyumba za wageni za bei kubwa. Ule Mfungasho ambao ulimtajia jina la Mwajuma Ndalandefu ukamwambia "Twende tu hapo nyuma kuna ya bei rahisi buku tano tu"…
Porokondo akaona ,, Nini bana… acha nikamalize fasta. Basi haoooo hadi kwenye hiyo gesti… Kufika pale kumbe ni zile gesti ambazo paa liko chini ambako kwa watu warefu kidogo inabidi ukunje shingo usiguse singibodi. Porokondo akazidi kunisimulia akasema, Mwajuma Ndalandefu fasta akasaula viwalo vyake na kuvitundika kwenye misumari iliyopigiliwa mlangoni na kasha kumuamuru Porokondo naye afanye hivyo wamalizane.
Wakaanza mambo yao vizuri, Porokondo wakati shughuli ikiendelea akaomba apatiwe mdundo wa mbwa kachoka, Mwajuma naye hakua na hiyana akageuka nae jamaa akasimama nyuma yake… Sasa taabu ikaja wakati anataka kumaliza mambo yake, Kwa mbwembwe akanyoosha mikono yake juu kama anashangilia fainali za kombe la dunia!!!! Hapa sasa ndipo makovu ya vidoleni yalipomkuta maana PANGABOI lililokua likizunguka darini likamchana chana vidole vyake vibaya sana.
Nilimuomba aishie hapo asiendelee kunihadithia maana hata hamu ya bia ikaniishia kabisa na nikamuaga nikaondoka nikisikitika huku roho ikiniuma.
FUNDISHO… Vijana oeni acheni mambo ya kununua.