Mwajiriwa achana na mikopo utajuta

floow

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
411
855
Habari wakuu,

Napenda kuwashauri wale ndugu zetu waliopata au wanaotarajia kupata ajira hivi karibuni suala la mikopo msilifikirie kabisa.

Kuna ndugu yangu yeye ni mwalimu alikaa mwaka mmoja tuu tangu alipo ajiriwa na kuchukua mkopo unaodumu miaka 4.

Alichopanga kufanya imeshindikana na pesa imeshapotea, matokeo yake haifurahii kazi yake.

Pesa nyingi ipo kwenye inakatwa take home imebaki pesa ya chips na tayari ana mke na mtoto kwa sasa anafikiria kuacha kazi mkopo unamtesa sana na maisha yamekua magumu sana.

Mikopo kero jamani futeni mawazo ya mikopo.
 
Habar wakuu
Napenda kuwashaur wale ndg zetu waliopata au wanaotarajia kupata ajira hiv karibuni...... Suala la mikopo musilifikirie kabisa

Kuna ndg yang yeye Ni mwalim.....alikaa mwaka mmoja tuu tangu alipo ajiliwa na kuchukua mkopo unaodumu miaka 4.....

Alichopanga kufanya imeshindikana na pesa imeshapotea, matokeo yake haifurahii kazi yake.... Pesa nying ipo kwenye makato take hom.... Imebaki pesa ya chips......na tayar anamke na mtoto........ Kwa sasa anafikiria kuacha kaz mkopo unamtesa sana na maisha yamekua magumu sana

Mikopo kero jamani futeni mawazo Ya mikopo

Uliwahi kumuuliza kwann malengo ya mkopo hayakutimia, mwambie akupe SWOT Analysis ya mkopo huyo.

Kwa mfano mie nilikopa 5M mwaka 2010, wakati natoka kusaini tu mkopo jioni take Baba yangu mzazi anafariki tena 1500km tokea humu nilipo, Unajua kilichotokea.
 
Umeshindwa kujenga hoja kabisaaa... Mshauri na raisi wako nchi iache kukopa.
 
Uliwahi kumuuliza kwann malengo ya mkopo hayakutimia, mwambie akupe SWOT Analysis ya mkopo huyo.

Kwa mfano mie nilikopa 5M mwaka 2010, wakati natoka kusaini tu mkopo jioni take Baba yangu mzazi anafariki tena 1500km tokea humu nilipo, Unajua kilichotokea.
Hebu tujuze tupate somo na sisi
 
Wapo wanaofanikiwa na wapo wanaofeli.
Wapo waliofanya maendeleo kupitia mkopo.
Unapochukua mkopo analyze yafuatayo:-
1.repayment capacity. Yaondoe makato ya mkopo kwenye kipato chako, then ondoa tena na gharama za kuish. Make sure haupat negative. If negative usikope.
2. Returns. Je mkopo unafaida?. Angalia faida na gharama ztokanazo na mkopo in issolation. Additional Benefit of credit -additional cost of credit.Borrow only if additional benefits zinazid additional costs.
3.Risk taking ability. Je unaweza kucarry risk zitokazo na mkopo?. Risk ni probability ya kufail.jaribu kuanalyse je unauwezo gan wa kujikinga na majanga ambayo yanweza kusababisha ugumu katika marejesho. Example kuugua, kufiwa, ukame ktk kilimo, anguko la kiuchum etc. Fanya scenario/sensitivity analysis.

Kila binadamu anatakiwa awe na mkopo at each point in time. Mkopo ambao unaendena na kipato chake, mkopo ambao umepembuliwa kiyakinifu bcz Mkopo ni pesa ya gharama nafuu.

Usitegemee kwa kias kikubwa mkopo kuanzisha biashara, kunatakiwa kuwe na right mixture. Ni vizur ukaanzisha biashara kwa asilimia kubwa na mtaji wako mwenyewe then ukaongeza portion ya mkopo kadir biashara inavyozunguka.
 
Huwezi kuendelea bila mkopo sembuse mataifa makubwa yana kopa ushindwe wewe
Tatizo je una busness plan? umefanya cost and benefit analyis ya huo mladi?
Sasa sio unakopa unataka kutembea na malaya wa mjin au ulete heshima baa au ununue asset,ujenge,sijui gali la kutembelea wakat mwisho wasiku utakua una lud na sh lak2 hom ndio kilicho bak kwenye mshahara.. na mafuta utapata wap?ndio mwanzo wa kusaga sori na gali lipo hom kwa sababu utakosa mpaka nauli ya daladala
Kopa hakikisha pesa inazaa pesa then wew unakula matunda ya mkopo
Nakwambia my friend unaweza sahau mshara ata miezi 6..kweli kabisa..sasa unakuta mladi una zalisha mil 4 kwa mwezi seklin unapata lak 2..si bonge la faida ktka kukopa..na usiache kazi kwani itakusadia kulipa deni na kukopa zaidi na zaid alafu watu wa bak kusema jamaa ana tumia kalumanzila au kwa prof.maji malefu
 
Habari wakuu,

Napenda kuwashauri wale ndugu zetu waliopata au wanaotarajia kupata ajira hivi karibuni suala la mikopo msilifikirie kabisa.

Kuna ndugu yangu yeye ni mwalimu alikaa mwaka mmoja tuu tangu alipo ajiriwa na kuchukua mkopo unaodumu miaka 4.

Alichopanga kufanya imeshindikana na pesa imeshapotea, matokeo yake haifurahii kazi yake.

Pesa nyingi ipo kwenye inakatwa take home imebaki pesa ya chips na tayari ana mke na mtoto kwa sasa anafikiria kuacha kazi mkopo unamtesa sana na maisha yamekua magumu sana.

Mikopo kero jamani futeni mawazo ya mikopo.
Hapa nilipo natoka kukamilisha taratibu za mkopo,nikamilishe nyumba ya kupangisha,nitapata 200,000/-kila mwezi,then kiasi nimeishafanya analysis nafungua biashara nitapata 50,000/-kila siku.kama nitakumbana na mkwamo kwenye biashara natarajia nyumba ieendelee kuni imarisha.Basi maisha yanaeenda.
 
Bila mkopo huwezi kutoka Mkuu, sema inategemeana na malengo ya mkopo wako so kabla hujakopa panga kitu cha kufanyia mkopo wako sio unakopa hafu unatafuta kitu cha kufanya utajuta.
 
Sasa kesi ya mtu mmoja unatoa hitimisho nawafahamu waajiriwa zaidi ya kumi wenye miradi,nyumba,familia na gari kwa sababu ya mikopo
 
Kukopa sio dhambi. Dhambi ni kutokua na hata busness plan ambayo ukikopa kama unakatwa kwenye mshahara hakikisha unafanya biashara ambayo inarudisha ike hela unayokatwa kila mwezi.
 
Hapa naona kuna makundi mawili,Wanaofagilia na wanaochikia.Kimsingi mtu yeyote anayechukua mkopo ana jambo analotaka kulitatua kwa wakati huo.KOPA KWA BUSARA LIPA KWA WAKATI La sivyo utajuta!!!
 
Mimi hata nikishauriwa na mtu aliyetoka mwezini niache kukopa benki, sitamsikiliza.
Mkopo ni mzuri kama una malengo na fedha unayokopa.
Ningekupongeza sana kama ungeshauri
Mtu asikope bila kuwa na mipango thabiti ya kufanya na huo mkopo.na pia kuangalia masharti unayopewa na mkopeshaji.
Kuhusu kuacha kazi,mimi niliwahi kuhama
Kampuni moja kwenda nyingine nikiwa na mkopo
Nilichofanya nilihakikisha mwajiri mpya nampa namba ya akaunti ya mkopo pia nikawajulisha benki kuwa nimebadirisha mwajiri.nililipa mkopo wangu nikimaliza bila shida.
 
Siku hizi kinachoumiza ni mikopo ya masomo ya elimu ya juu
Ambayo imeingilia katikati ya mikopo ambayo watu walikopa kwenye mabenki.
Hakuna benki inayokukopesha bila kuangalia mshahara wako Kama utakuwezesha
Kulipa deni na maisha yakaendelea Kama kawaida. Hata kama umeomba mkopo mkubwa unapewa Sawa sawa na uwezo wako wa kulipa. Hili la kubaki na hela ya chips mmmmm!!
 
Back
Top Bottom