Mwafrika bado kalala!

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,589
1,679
Kila mtu mwenye akili anayefuatia yanayojiri duniani ataweza kung'amua haraka kuwa kuna maandalio makubwa na ya haraka ya vita kuu ya tatu. Ukitazama hali ya mahusiano ya kimataifa ilivyozorota: ubabe wa Marekani unavyozidi kwa kukita makombora mlangoni mwa Urusi, kutibua makubaliano ya kiungwana 'gentleman's agreement' yaliyofikiwa wakati wa Soviet Union ya kupunguza zana kali za kivita, kuvamia na kutwaa maeneo zaidi ya nufudhi 'sphere of influence' ya Urusi.....

Hayo pamoja na maandalio yasiyo simile ya kutengeneza silaha yanayofanywa na madola kama China, India, Brazil n.k. utaona kuwa vita vya tatu vya dunia vinakuja, na huenda vikawa karibu. Nimeona nchi nyingi katika mabara yote isipokuwa bara la Afrika zina 'habari hii' na hivi sasa ziko mbioni kujipanga. Isipokuwa Afrika ambayo haina habari na hakuna dalili zozote za kuonesha viongozi wetu wana mwamko wowote wa hili.

Afrika ambalo ni bara lililoteseka zaidi kuliko mabara yote kwa ukatili na uhuni wa Wazungu, ungedhania ingekuwa msitari wa mbele kufikiria namna ya kujihami na madhara hayo katika mustakbali. (Biashara ya utumwa pekee ilipelekea kuuawa kwa watu milioni 20 Waafrika kutokana na taabu, sulubu na mateso wakati wa kuvuka bahari kuu za Atlantiki na Pasifiki. Na hata leo, vita vinavyochochewa na Wazungu vinaendelea kumaliza watu- vita vya Congo pekee tangu mwaka 1995 hadi sasa vinakadiriwa kuteketeza roho milioni 5 za Waafrika).

Labda ni kwa sababu viongozi wa Afrika wanawaamini sana hawa wazungu kuwa hawawezi kufanya unyama (sijui kwa nini). Wengine hata wanawaona kama mama na baba zao kiasi wakipata matatizo kidogo wanawakimbilia na kuwalilia! Kana kwamba mapambano yote yale ya uhuru na kujikomboa hayakuwa na shabaha yoyote ya kutufanya tuwe mabwana wa majaaliwa (destiny) yetu!

Natoa wito kwa viongozi wa Afrika wakutane haraka sana na waweke mikakati ya kujihami katika vita kuu ya dunia ijayo, kwa pamoja na kama nchi moja moja. Nchi ziweke mipango ya kuwahaami raia zake kama vile kuchimba mahandaki chini ya nyumba, hasa katika miji, kuweka chakula cha dharura, n.k. Miji mingi ya Afrika haina himaya ya watu kwa ajili ya vita.

Vita vya tatu vya dunia, tofauti na vita mbili zilizopita, vitapiganiwa zaidi katika nchi zinazoendelea kwa madhumuni ya kutwaa rasilmali ambazo zinazidi kupungua. Kama una shaka na haya, jaribu kusoma historia ya sababu zilizopelekea kuzuka kwa vita ya kwanza na ya pili ya dunia.
 
Huu utafiti wako umeufanya wapi?Kwanza hiyo vita ni mawazo yako,unataka watu wawe bize na nadharia zako?Thibitisha kwanza unachosema halafu ndo ulaumu watu kwa kutokutilia maanani fact siyo nadharia!
 
Sishangai, ikiwa rais wako hayajui haya, sembuse wewe? Nimekuletea picha fupi ya casus belli, wataka nini tena? Ni juu yako kuthibitisha ikiwa hayo hayapo.
Hello?????
 
Acha Bwana kueneza chuki binafsi DHIBITISHA usemi wako huo Rais wako haya unayoyasema hayajui wewe umeyapataje???????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom