Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,733
- 40,846
Sakata la Richmond na mtikisiko wake bado havijaisha Bungeni. Kuna kila dalili kuwa yaliyotokea Bungeni mwezi wa pili na kusababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na kuvunjika kwa baraza la Mawaziri hayakuwa mwisho. Kuna kila dalili kuwa kuna baadhi ya watu ambao waliumizwa na hadi hivi sasa hawajakubali "yaishe"
Miongoni mwa watu ambao kwa hakika waliumizwa hisia zao, hadhi na sifa zao ni Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz (CCM) ambaye wakati wa matukio hayo alidai kuwa ripoti iliyosomwa na Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge Mhe. Harrison Mwakyembe (Kyela - CCM) haikuwa sahihi na akadai kama vile wengine kuwa hakutendewa haki.
Juhudi za kujisafisha kwa wahusika mbalimbali wa Richmond zimekuwa zikiendelea na kwa namna fulani jukumu kubwa zaidi linamuangukia Bw. Rostam ambaye aidha kwa kujitwisha mwenyewe au kukubali kutumika inaonekana amekuwa akitumia kila aina ya njia upande mmoja kujibu mashambulizi ya wapinzani kwa kutumia vyombo vyake vya habari na upande wa pili kutilia shaka utendaji mzima wa Kamati Teule na hivyo kujaribu kuhoji maamuzi yote yaliyotolewa Bungeni
Katika kikao kinachoendelea cha Bunge alitakiwa aje kutoa maelezo yake na kujibu hoja za Wabunge na kutoa utetezi wake. Mwishoni mwa juma alikuwa amejiandaa kutoa utetezi huo lakini kwa kile kinachodaiwa kuwa ni "unyeti" wa utetezi wake basi imeonekana si vyema kwa Bw. Rostam kujitetea Bungeni kwani italeta msukosuko mwingine nchini
Kama hilo ni kweli au ni mojawapo ya karata za CCM binafsi siamini kuwa Rostam anaweza kusema chochote kile ambacho kinaweza kutuyumbisha kama Taifa na ambacho hatuwezi kukihimili. Tumeweza "kuchafuka kwa hali ya kisiasa Zanzibar", tumeweza kuhimila msiba wa Sokoine, tumeweza kuhimili "mizengwe" ya Kizota na kifo cha Katibu Mkuu Kolimba na kwa hakika tumeweza kuhimila kujiuzulu kwa WAziri Mkuu
Naamini nchi yetu inaweza kuhimili msuko suko wowote ule wa kisiasa hata kama ni kujiuzulu kwa Rais aliyeko madarakani! Hata ikibidi Bunge zima kujiuzulu au kuvunjwa na kuitisha uchaguzi mwingine, TAifa letu lina uwezo wa kuhimili mambo hayo kwani Taifa ni kubwa zaidi kuliko kikundi fulani cha wanasiasa.
Wito wangu leo ni kuwa kama Rostam analo la kusema na aliseme sasa asinyamazishwe tena wala kupigwa mkwara na chama chake. Kamas anaona hakutendewa haki yeye kama Raia basi anayo haki ya kujisafisha hadharani badala ya kulazimika kukaa kimya. Asije akafikiri kuwa ana mpango wa kuzungumza "huko mbeleni" lakini ikatokea kuwa yeye na utetezi wake wakanyamaza "milele" kama alivyonyamaza Bi. Amina Chifupa ambaye naye alitaka kupewa nafasi ya kujitetea lakini akazibwa mdomo. Natoa wito; kama Rostam unaamini una hoja SIMAMA JITETEE NA JIELEZE usikubali kufungwa na Ibara ya 15:1 ya Katiba ya CCM
Lakini swali kubwa ni Rostam ana nini ambacho kinampa nguvu ya kutia mwashawasha Bungeni? Je anatikisha kiberiti kuona kama kimejaa