Mwache mchagga aitwe mchagga

Mwache mchagga aitwe mchagga

Sema tu umecopy toka gazeti la the nation..hii kitu ilitokea Nairobi na mfanyabiashara alikuwa anaenda Dubai... Siku nyingine ukidanganya tumia akili kidogo
 
MWACHE MCHAGGA AITWE MCHAGGA
Jamaa mmoja toka kiboriloni alienda Benki na kuomba mkopo wa shilingi 200,000 ili asafiri kwenda Dar. Ofisa mikopo akamwambia lazima ajaze fomu fulani na awe na kitu cha kuweka dhamana. Mdau akajaza fomu kisha akakabidhi funguo za benzi yake aliyokuja nayo pamoja na nyaraka za umiliki wake kwa meneja. Ofisa mikopo akaiingiza gari kwenye yadi ya benki na kumpa mchagga laki mbili yake. Kilichomshangaza meneja wa benki ni kuwa benzi ile ina thamani ya 255,000,000 na kuwa iweje mwenye gari kama hii amekosa 200,000. Baada ya wiki 2 mchagga akarudi na kurejesha mkopo wote pamoja na riba ya shilingi 15,000. Afisa mikopo akafurahi lakini akamuuliza, inawezekanaje una gari la thamani hivi na ukahangaika kupata mkopo wa shilingi laki 2? Mchagga akamjibu, Ni wapi hapa Moshi utapata mahali salama kupaki gari yako kwa wiki mbili kwa kodi ya shilingi 15,000 tu?
Umetafsiri na kuhariri ile ya Mmasai wa Nairobi iliyokuwa imeandikwa kwa kiingereza, na kuifanya ya Mchaga wa Moshi. Utakuwa Mchaga ww, hongera kwa falsafa ya mwamba ngozi...
 
Hakuna benki inatoa mkopo kwa utaratibu huo.Km gari ilikuwa dhamana, wanahitaji tu kadi ya gari na siyo gari wala funguo
Dah.... Chief ungekutana na stori za "Sungura akasema....." nadhani ungezimia
 
uwe na benzi ya 255,000,000 ukose pa kulilaza ooh but an away kumbe ni story tuu
Hutakosa pa kulaza benzi lakini je hap mahali ni salama? Kule benki ni salama kwanza kwasababu ya walinzi imara, pili hata kama gari ikiibiwa ikiwa mikononi mwa benki utalipwa gari nyingine, ujanja huo mkubwa mno kwa 15,000/=!
 
Back
Top Bottom