GE2025 Mwabukusi: Rais Samia aliniambia suala la Lissu watalishughulikia bila kuingilia utaratibu wa mahakama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kushughulikia mambo mbalimbali aliyoyawasilisha kwake alipozungumza nae Ikulu Dodoma.

Akijibu swali kuhusu majibu ya Rais Samia kama alizungumza na kuhusu kesi ya Tundu Lissu, Mwabukusi alisema kuwa jambo hilo aliliwasilisha na Rais Samia alimuahidi kulishughulikia katika namna ambayo hawataingilia taratibu za Mahakama.

"Na nilitoa taarifa kama tumezungumza na Rais alisema wanalishughulikia, ametusikiliza na aliniambia kuna wengine walifika mbele yake aliwasikiliza na watalifanyia kazi bila kuingilia utaratibu unaoendelea Mahakamani," alisema Mwabukusi

Aidha Wakili huyo aliendelea kusema kuwa, katika mazungumza hayo na Rais Samia hawakuzungumza tu suala la Lissu, bali yapo mambo mbalimbali waliyawasilisha kwake ikiwemo watu kupotea na Demokrasia na Utawala bora.

"Suala la Lissu ni moja ya mambo tuliyoyawakikisha kwa Rais, sio Lissu tu yapo mambo ya Demokrasia na utawala Bora, Sheria za uchaguzi na kanuni zake, suala la watu kupotea na suala la msomi Wakili Tundu Antipas Lissu," alisema Wakili Mwabukusi

Mwabukusi ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa Habari, alipofika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam kufuatilia kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu.
 
Lissu lazima atadai fidia kubwa tu.
Hata mimi ndio kitu ninachokiona. Lissu anataka aache FUNZO kubwa kwa vizazi vijavyo kwamba si tu Aliigaragaza Serikali kwenye Kesi ya UHAINI bali pia na kuilazimisha kumlipa FIDIA kwa Kum defamate kwa kesi isiyo na K wala M chafulia, jina, Kumpotezea Haki yake ya kushiriki mambo ya kisiasa kipindi cha Uchaguzi nk
 
Na sio mahakama Tena?
Anapelekwa huko ili iwe nini kama MAAMUZI hayatoki mahakamani?


Fullstop, kwishaaaa
 
Washughulikie hilo mapema atoke,tunamtaka aje kugombea.
 
Kutoka viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam tunakusogezea kuona jinsi msafara uliomleta Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu alivyoingia Mahakamani hapo mapema leo, Jumatano Septemba 10.2025 Lissu ambaye amefikishwa Mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa Jeshi la Magereza, ameletwa kwa ajili ya mwendelezo wa kesi ya uhaini inayomkabili ambapo Mahakama chini ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Ndunguru kwa siku ya tatu mfululizo inaendelea kusikiliza mapingamizi yaliyowasilishwa na mshtakiwa.


Your browser is not able to display this video.
 
Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi ameeleza kuwa ameliwasilisha jambo la Lissu kwa Rais na aliahidi kulifanyia kazi, ameyasema hayo Wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama Kuu wakati akielekea kwenye kesi ya uhaini inayomkanili Tundu Lissu.

"Nilisema Rais alisema wanalishughulikia, ametusikiliza na aliniambia hata wengine wamefika mbele yake aliwasikiliza. Watalifanyia kazi kwa utaratibu ambao hautaingilia utaratibu unaondelea mahakami" - Boniface Mwabukusi, Rais TLS
Your browser is not able to display this video.
 
Maana yake atakuwa convicted halafu atoke kwa msamaha wa Raisi mwishoni huko wa kipindi chake kuisha katika ile siku ya kumbukizi ya Muungani 26/04. Ndivyo nilivyo elewa mimi...au wewe unaonaje ?
 
Sasa wangemtoa mapema kabla Mrema na Katuga hawajaonyesha ni kiasi gani hawana umakini. Especially Mrema ambaye anakula mshahara bure.
 

Tangu lini maneno matupu yakavunja mfupa?

Angalizo la Polepole la Wahuni kuwa kila mahali linaonekana kutoeleweka bado. Hata upinzani, Sauti ya Tanzania, TLS, nk, ni dhahiri kuwa nako wapo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…