Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Nimeshtushwa mno na shambulio la kikatili linalokosa misingi ya utu na lisiloweza kuelezeka mbele ya jamii yeyote uenye watu timamu.
Ni msingi wa Kisheria na Kikatiba kwamba:
1. Mahakama ni chombo huru kinachopaswa kufanya kazi bila mashinikizo, vitisho au uingiliaji wowote kutoka kwa vyombo vingine vya Dola. Polisi kuzuia wananchi kuhudhuria kesi ni sawa na kudhibiti mazingira ya kimahakama kinyume na Katiba (ya Jamhuri ya Muungano).
Wajibu huo unatakiwa kulindwa na Mahakama yenyewe kupitia hakimu anayeendesha kesi husika. Lazima haki ionekane ikitendeka
2. Wananchi wana haki ya kikatiba, kisheria na kidemokrasia ya kushuhudia mwenendo wa mashauri mahakamani, ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji.
Soma Pia: Kutoka Mwananyamala Hospitali: Viongozi wa Chadema Waliovunjwa Miguu hawa hapa
Kuzuia haki hii bila kuwepo kwa msingi wa kisheria wala kikanuni na kutafuta njia mbadala zinazo zuia haki ya wananchi kushujudia na kuona haki ikitendeka ni kuzuia ushiriki wa umma katika mchakato wa haki.
3. Wananchi wakikusanyika kwa amani kwenda kushuhudia kesi, basi kuwakamata au kuwaumiza na muwatupa porini ni ukiukaji wa haki yao ya kikatiba ya kukusanyika na kujieleza.
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) tumekuwa tukisisitiza na kukemea ukiukaji huu wa sheria na matumizi mabaya ya kisheria.
Tuneielekeza Kamati ya TLS kukaa na kuona namna bora ya kushughukikia jambo hili kwa uzito na njia zinazostahiki.
Tunatoa pole kwa waathiriwa wote wa vitendo hivi vya kikatili vilivyotendwa dhidi yao na pia tunawashauri.
1. Kwenda Polisi Mara moja wapatiwe PF 3 ni haki yao.
2. Wale wanaokataliwa wawekeke kumbu kumbu kumbu ya barua au ushahidi husika ikiwemo picha na Madhila waliyo pata.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivi na kuonekana kuanza kuota mizizi na kuzoeleka TLS itaona namna bora ya kushirikiana na waathiriwa katika kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa taasisi na kila muhusika kwa jina lake kuona namna kamilifu ya kushughulikia jambo hili baada ya kupata taarifa kamili kutoka kwa kamati husika.
BAK Mwabukusi
Rais TLS
Rais - TLS.