Mvutano wa RC na Pastor

Mvutano wa RC na Pastor

Pasta katuhumiwa uwongo wakamwachia baada ya kukosa ushahidi hivo yupo kifua mbele kueleza anavoonewa wivu na viumbe wa Mwenyezi Mungu.
Hivi ninyi watu nawastaajabu sana aina ya ushabiki wa kujifyetua akili mlionao wakati huu wa kipindi hiki kigumu.
Hivi kupekuliwa na kukosekana kithibiti kinamsafishaje mhusika kuwa hashiriki uhalifu huo?
Mara ngapi majambazi wanaofahamika katika jamii kuwa ni majambazi, wamevamiwa kupekuliwa tena ghafla na hawakukutwa na kithibiti. Je hao siyo majambazi kwa kuwa hawajakutwa na kithibiti?
Kulikuwa na uadui gani kati ya Makonda na Gwajima hadi Makonda amtaje Gwajima kama njia ya kumkomoa?
Magwiji wengi wa biashara ya dawa za kulevya ama uhalifu mwingine wowote mkubwa hujificha katika nyadhifa mbalimbali za kidini, kisiasa ama kiserikali , kutumia uheshimiwa kama kichaka cha kuhifadhia mabaya katika macho ya jamii. Hayo siyo ya mfano, hayo ni mambo halisi tuliyoyashuhudia yakitokea.
Nadhani tungejiuliza hapa huyo sijui Bishop kwanini alitajwa? Wadhifa wa aina yoyote ama kupekuliwaha na kukosekana kithibiti haizuii mtu kuwa mhalifu.
Tumeshuhudia hadi rais wa nchi akituhumiwa kushiriki katika biashara hiyo haramu,sembuse baba askofu?
Toa sababu za kimantiki kwamba kwanini hahusiki moja kwa moja na siyo kueleza sababu zisizokuwa na mashiko kwamba kapekuliwa na hakukutwa na kithibiti kwa hiyo hahusiki.
 
Njia iliyotumika haijawahi leta matokeo duniani zaid ya kukimbiza ushahidi, ukimtuhumu MTU ili iaminike unaweka ushahidi
 
RC wetu akitoa cheti chake cha Kidato cha nne,Maadui wake wote watayeyuka! Rais Obama ndivyo alivyofanya,baada ya watu kuzusha kwamba alizaliwa Kenya!
 
Back
Top Bottom