Mvutano mkali wa kisheria waibuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvutano mkali wa kisheria waibuka

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by jamadari, Apr 28, 2010.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  28th April 2010


  [​IMG]
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Absolom Mwakyoma.  Vuta nikuvute iliibuka jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Kilimanjaro juu ya kuletwa nchini na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria mtuhumiwa Patrick Ais Ingoi, raia wa Kenya katika kesi ya wizi wa zaidi ya Sh. bilioni 5.3 mali ya benki ya NBC tawi la Kibo, mjini hapa.
  Mvutano huo ulikuwa baina ya mawakili wa upande wa mashtaka na utetezi baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la kuiombamahakama hiyo kutoa amri ya kuletwa nchini kwa mshtakiwa huyo na kuunganishwa na washtakiwa wenzake tisa wakiwemo raia wanane wa Kenya na Mtanzania mmoja, ombi ambalo lilipingwa vikali na upande wa utetezi.
  Kesi hiyo ililetwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Gabriel Shayo, kwa kusikilizwa.
  Jumla ya mashahidi wanne akiwemo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Absolom Mwakyoma, walifika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.
  Wakili Mwandamizi wa Serikali, Biswalo Mganga, akisaidiana na mawakili wa serikali, Stella Majaliwa na Ladslaus Komanya, alidai kuwa Mahakama Kuu nchini Kenya ilishatoa amri ya kuletwa nchini kwa mtuhumiwa huyo lakini wakati taratibu za kumleta nchini zikifanyika, alikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa nchini humo.
  Pia alidai kuwa wamepata taarifa kutoka ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali ya Kenya (DPP) kuwa mawakili wa utetezi katika kesi hiyo walipeleka taarifa kuwa mtuhumiwa huyo hana kesi ya kujibu.
  “Kutokana na sababu hizo, itakuwa vigumu kwa Mahakama ya Rufaa kufikia uamuzi hadi ipate uthibitisho kutoka Tanzania kuwa huyu mtu bado tunamhitaji na ana kesi.
  Tunaomba mahakama itoe amri ya kumuita kwani ni miongoni mwa washtakiwa muhimu katika kesi yetu, tunaomba kesi iahirishwe na tupate hati ya kumleta mahakamani Patrick,” alisema Wakili Mganga.
  Hata hivyo, wakili wa utetezi, Loom Ojare, alisema wanapinga kwa nguvu zote ombi hilo kwa kuwa jalada la kesi namba 40 ya mwaka 2006 lililopo mahakamani hapo, limemaliza miaka minne na miezi minne na hati ya mashtaka na jalada hilo hakuna mahali kunaonyesha jina la Ingoi kama ni mshtakiwa katika kesi hiyo.
  Alidai kuwa ombi hilo limekuwa kinyume cha utaratibu wa sheria, ambao unasema mtu anayeshtakiwa mbele ya mahakama ashtakiwe kwa hati rasmi inayotaja jina kamili, kosa analoshtakiwa nalo na maelezo ya kosa analodaiwa kutenda.
  Alidai Wakili wa Serikali hajatoa nakala ya hukumu ya Mahakama Kuu ya Kenya iliyoamuru mshtakiwa huyo arejeshwe Tanzania, matokeo ya rufaa hiyo, pia hajaeleza taarifa iliyopelekwa kwa DPP wa Kenya ilipelekwa kwa njia ya simu au kwa karatasi na hata kama ni kweli ilipelekwahakuna hati yoyote iliyopo mbele ya mahakama hiyo inamhusu Ingoi.
  “Mahakama tukufu ni mahakama ipasayo kufuata sheria katika utendaji wake wa kila siku na siyo kusikiliza maneno yasiyo na uthibitisho wowote, tulitarajia kama upande wa mashtaka upo makini na tuhuma dhidi ya Ingoi ungewasilisha kumbukumbu zote zinazohusu kuhitajika kwa mtu huyo pamoja na hati ya kumkamata,” alieleza.
  Wakili Ojare, alidai upande wa utetezi unaona kuwa maombi hayo yamekuja ili kuchelewesha usikilizwaji wa kesi hiyo kwa lengo lakuwatesa washtakiwa ambao wameshateseka kwa miaka minne bila kesi yao kusikilizwa na kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali ombi hilo na kuendelea na usikilizaji wa kesi.
  Aidha, mshtakiwa wa 10 katika kesi hiyo ambaye ni raia pekee wa
  Tanzania na anajitetea mwenyewe, Askofu Jumanne Chilongola, alidai washtakiwa hao wapo mbele ya mahakama hiyo kwa mujibu wa sheria na kwamba si mara ya kwanza upande wa mashtaka kuleta ombi kama hilo na kama wangeamua kumleta wangekwishafanya hivyo ila wanachofanya ni kuongeza siku za mateso juu yao.
  “Kesi hii ni marudio ya kesi nyingine ya mwaka 2004 iliyokuwa inawakabili raia wa Tanzania na ilishatolewa hukumu, kwa kuwa mahakama hii ipo kisheria, tunaomba ikatae ombi hili...walikubali kesi hii isikilizwe kuanzia Aprili 27 hadi 30, mwaka huu, leo wanaleta hadhithi za Ingoi kuletwa nchini, ombi kama hili walishalileta na liliwekwa kando na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya, Ruth Mkisi,” alisema.
  Akijibu hoja hizo, wakili wa serikali, alidai kuwa ucheleweshaji wa kesi hiyo umechangiwa na pande zote mbili kwani washtakiwa hao wamekuwa wakikata rufaa mara kwa mara na hadi sasa wanapinga kesi hiyo kusikilizwa na mahakama hiyo.
  Wakili Mganga alidai kuwa madhara ya kutomleta Ingoi ni kusababisha mashahidi kurudia rudia kutoa ushahidi wao.
  Hata hivyo, Hakimu Shayo alisema atatoa uamuzi Aprili 30, mwaka huu, ili kupata muda wa kutosha kupitia jalada hilo kwa kuwa kesi hiyondio imeletwa kwake kwa mara ya kwanza.
  Tukio la uporaji ndani ya benki hiyo lilitokea Mei 21, mwaka 2004, ambapo kundi la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, walipora Sh. bilioni 5.3 mali ya benki hiyo.
  Kufuatia wizi huo,watu 14 walikamatwa na kufunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Biashara wakati huo ambapo Jaji Amir Mruma alitoa hukumu Desemba, mwaka 2006.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 765
  Likes Received: 550
  Trophy Points: 180

  Mvutano wa kisheria uko wapi hapo unaostahili kichwa cha habari hicho? Naona ni pande mbili kila moja ikitoa hoja na mapingamizi ya upande wao. Hiki kigazeti cha Nipashe sikinunui hata siku moja!
   
Loading...