wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,931
- 4,550
Wakuu,kijana mmoja aliyekuwa ameanza kujifunza kuvuta bangi,ktk eneo la Runzewe lililopo ktk barabara ya Burundi na Rwanda leo amejikuta ktk hali ngumu baada ya kuvuta bangi na kisha kuvaa vazi lenye muonekano wa mbuzi na kisha akajichanganya na kundi la mbuzi hao huku akiwa kavaa vazi hilo linalosemekana alilinunua mtumbani,kijana huyo huku akiigiza kama mbuzi alilivamia kundi la mbuzi kwenye malisho yake akawa anajifanya na yeye ni mbuzi,kisha akaanza kutaka kumpanda mbuzi jike,mchungaji wa mbuzi wale hakuweza kushtuka hata kidogo,ndipo yule kijana alipomparamia mbuzi jike ili kumbaka,kuona vile mabeberu ya mbuzi yakajawa wivu na kumvamia yule kijana,alikimbia kimbuzi mbuzi,alipoona mambo mazito,aliamua kukimbia kibinadamu lakini bado wale mbuzi hawakumuacha,zaidi ya mbuzi 20 waliendelea kumfukuza,ni tukio ambalo limeacha gumzo kubwa sana ktk mji huo mdogo,na alikokimbilia yule mvuta bangi hadi sasa hapajulikani,ila taarifa zinasema kuwa bado yuko porini hadi sasa hivi,ndo alikuwa anajifunza bangi.