Mvua yazidi kuleta maafa, sasa yaua Morogoro

Mvua yazidi kuleta maafa, sasa yaua Morogoro

Tina

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2007
Posts
572
Reaction score
584
Siku chache baada ya Malaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutoa tahadhari ya kuwapo mvua na upepo ikiutaja mkoa wa Morogoro kuwa miongoni mwa maeneo hatarishi, tayari mvua hizo zimesababisha maafa kwa kuua mtu mmoja , kuharibu nyumba 127, majeruhi tisa (9) katika maeneo ya kata za Kisaki na Mngazi.... ambako mvua yenye upepo na radi.

Taarifa za awali za TMA hizi hapa:

https://www.jamiiforums.com/habari-...-mvua-kubwa-upepo-mkali-mawimbi-baharini.html

Na huko Kigoma nako yalitokea:

https://www.jamiiforums.com/habari-...usuru-imezama-na-watu-9-wamefariki-dunia.html
 
Taarifa kutoka kwa PESSA M PESSA DIWANI BWAKIRA CHINI, Morogorogo zinaeleza:

Siku ya j,mosi th 05.01.2013 saa tisa alasri ktk kata ya KISAKI na MNGAZI kumetokea MVUA yenye RADI na UPEPO mkali ilyoharibu NYUMBA 127, MAJERUHI 9, na KIFO 1. Majina ya vijiji na idadi ya nyumba ni SESENGA KATA MNGAZI 1, GOMERO KATA KISAKI 81, KICHANGANI KATA KISAKI 15, KISAKI KITUONI KATA KISAKI 30. Pia RADI imemuua mama mjamzito TERESIA GAITANI 27, na kumjeruhi mume wa marehemu aitwae ATHUMANI KILUKE 36.

"WALIOJERUHIWA NI MOHAMED KIDWANGA,HABIBU SALEHE,HASSAN ALLY,ALLY KIBUSUKE,ALIFA ABDALAH(MTOTO),ZAINABU MUHAMO,SAIDA ABDALAH NA AMINA ABDALLAH /MTOTO"
 
poleni wafiwa. RIP marehemu
 
Back
Top Bottom