Mvua yasababisha maafa Mtwara

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,249
2,000
Baadhi ya wakazi wa Kiangu na Chuno mjini Mtwara wamelazimika kuyahama makazi yao yaliyojaa maji baada ya mvua kunyesha.

Mvua ilinyesha usiku wa kuamkia jana Jumamosi Desemba 9,2017 saa nane usiku pasipo kukata hadi saa kumi na moja jioni. Mvua ilikata kwa muda na kuendelea kunyesha usiku hadi leo Jumapili Desemba 10,2017.

Katika maeneo hayo MCL Digital imeshuhudia wananchi wakiokoa mali zao ambazo zilikuwa zimelowa.
Miongoni mwa mali zilizoharibika ni magodoro, samani, majokofu na televisheni. Baadhi ya vijana wamekuwa wakiwasaidia wazee kuhamisha mali na kuwaondoa maeneo yaliyozingiwa maji.

Mkazi wa Kiangu, Edith Mboni ameiomba Serikali kujenga mitaro itakayopeleka maji baharini ili kuwaondolea adha hiyo. Amesema mtaro uliopo ni mdogo hivyo kutokana na wingi wa maji unashindwa kuhimili.

Mkazi mwingine, Hassan Mbarali ameiomba Serikali kujenga miundombinu imara ili kuwaepusha na maafa ambayo yamekuwa yakijirudia mvua kubwa inaponyesha.

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Desemba 8,2017 ilitoa taarifa kwa umma ikieleza kuwapo vipindi vya mvua kubwa katika maeneo ya ukanda wa Pwani.

Maeneo hayo ni mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba.mwananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom