Mvua kubwa yasababisha maafa Sierra Leone

Mvua kubwa yasababisha maafa Sierra Leone

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, imeongezeka na kufikia zaidi ya watu mia tatu.

Inaofiwa kwamba miili zaidi iko chini ya vifusi.

Jitihada za kuokoa zilisitishwa kwa muda baada ya giza kuingia. Rais Ernest Bai Koroma amesema kupitia televisheni kwamba vituo vya dharura vimewekwa ili kukabiliana na kile alichokiita janga la taifa.

_97332688_c4bfec98-39f3-4d6b-956c-a19584a39bca.jpg


Shirika la Msabala mwekundu limesema inakadiriwa zaidi ya watu laki tatu wamepoteza makazi yao.

Eneo lililoathirika zaidi wilaya ya Regent iliyopo pembezoni mwa mji wa Freetown baada ya mlima uliojaa maji kuporomoka.
 
Duu pole zao.Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi.
 
Duu pole zao.Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi.
 
Navuta picha jinsi mtu alivyopambana kujenga nyumba yake ya thamani kwa muda mrefu tangu akiwa kijana hadi amefikia umri mkubwa sasa anataka kuinjoy na familia yake matunda yake lakini kufumba na kufumbua hakuna nyumba na kiwanja chenyewe cha kupapasa dah, Mungu turehemu sisi wanadamu tuishio katika Dunia yenye laana.
 
Back
Top Bottom