Mvua kubwa yaja

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,456
Reaction score
872,092
Mvua kubwa yaja, TMA yatoa tahadhari ya siku tano

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya siku tano ya kunyesha mvua kubwa inayoweza kusababisha athari ikiwemo mafuriko.

Mvua hiyo inatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

Kwa mujibu wa TMA, mvua hizo zinatarajiwa kuanza kunyesha leo Ijumaa Machi 29 hadi Aprili 2, 2019 na kwamba zinaweza kuleta athari kwenye makazi ya watu.

Pia, kuleta shida katika usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Mamlaka hiyo imesema kuanzia leo hadi Machi 31, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na Morogoro.

Imesema Aprili Mosi hadi Aprili 2, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

TMA imeshauri menejimenti ya maafa, watoa huduma za dharura pamoja na wadau wengine kuchukua hatua za kuweka mipango stahiki kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.


Chanzo: https://mobile.mwananchi.co.tz/Haba...97580-5047982-format-xhtml-l4neoyz/index.html

Jr[emoji769]
 
Mwaka huu ngoma ngumu..wakulima imekula kwetu! Kuna mbwa Jana nimshuhudia analamba reli..tunakoelekea tutaanza kuchemsha viatu vya ngozi na mikanda tupate supu..hatari fire!
 
Afadhali hata mvua ije maana Mshana jr kwenye zile shughuli zenu za kuruka naight mtaenda likizo fupi😀
 
Mbona hawakutaja visiwa vya MURUTUNGURU ndani ya Ukerewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…