Mvua Kilimanjaro: Kaya zaidi ya 2,200 hazina mahali pa kuishi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Zaidi ya kaya 2200 katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro hazina mahala pa kuishi, wala chakula na mahitaji mengine muhimu ya kibinadamu.

Maafa hayo yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo na kusababisha maafa makubwa ya vifo, pia uharibifu wa mali na mashamba.
13051631_963179670446375_8120617100271568732_n.png
 
yaa mkuu taharifa ya itv juzi walisema watu 7 walidondokewa na nyumba zao jana ndio niliskia mkuu wa wilaya angeenda kutathmini naona mrejesho hatujapewa tena..
 
YALE MAENEO NI HATARISHI MIAKA YOTE LAKINI WATU NI VICHWA NGUMU. NA KILA MARA MVUA ZIKINYESHA LAZIMA WAATHIRIKE.

KWA NINI WASIHAME????????????
 
Haya wanaume wa huko mutoe misaada sio mumesimama tu hapo mumeshika viuno
 
Kuna kijiji kinaitwa Chemchem kiko kata ya Arusha chini/TPC Wilaya Moshi kimezoea kukumbwa na mafuriko kila mwaka,kimegeuka kuwa kisiwa ndani ya nchi kavu,hakuna barabara inayoingia wala umeme.
 
Hakuna Wilaya ya Moshi

Kuna Moshi Mjini na Moshi Vijijini..

Unaweza kunitajia mkuu wa wilaya ya Moshi mjini na mkuu wa wilaya ya Moshi vijijini? Narudia tena, kuna wilaya ya Moshi (hakuna hiyo mjini wala vijijini), mkuu wake wa wilaya ni Novatus Makunga. Katika majimbo ya uchaguzi ndipo kuna jimbo la Moshi mjini (Mbunge wake ni Mh. Jafary) na jimbo la Moshi vijijini (Mh. Komu).

Kumbuka pia kuna Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi (hakuna wa mjini wala vijijini), ila kuna mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi. DAS (District Administrative Secretary) aliyepo ni mmoja tu wa Moshi (hakuna mjini wala vijijini). OCD ni mmoja tu wa Moshi (hakuna wa mjini wala wa vijijini). Natumaini utakua umeelewa.
 
Mkoa wa Kilimanjaro una Wilaya 6 na Majimbo 9 ya Uchaguzi

1. Wilaya ya Hai

2. Wilaya ya Moshi Mjini

3. Wilaya ya Moshi Vijijini

4. Wilaya ya Mwanga

5. Wilaya ya Rombo

6.Wilaya ya Same

Majimbo ya Uchaguzi

1. Hai - Freeman Mbowe
(CHADEMA)

2. Siha - Dr. Godwin Mollel
(CHADEMA)

3. Moshi Mjini - Ndg. Jaffary
Michael (CHADEMA)

4. Mwanga- Prof. Jumanne
Maghembe(CCM)

5. Same Mashiriki- Nagenjwa
Kaboyoka (CHADEMA)

6. Same Magharibi - Mathayo
David (CCM)

7. Moshi Vijijini- Anthony
Calist Komu (CHADEMA)

8. Vunjo- James Mbatia
(NCCR)

9. Rombo - Joseph Selasini
(CHADEMA)
 
Back
Top Bottom