Mvua katika jiji la dar ni baraka au kero

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Mvua iliyonyesha siku mbili tu katika jiji la Dar es Salaamu imeanza kuleta kero kwa watu. Mitaro imeanza kuziba, watu wa maeneo yasiyopimwa wameanza mtindo wa kuzibua vyoo vyao na marundo ya taka yamejaa katika maeneo mbalimbali ya barabara zetu. Barabara ya Morogoro maeneo ya Manzese Darajani kila kukicha kumejaa mizigo ya taka.

Kwa hali hiyo tutegemee magonjwa ya milipuko kama kipindupindu, kuhara na magonjwa ya tumbo, pia malaria kwani mvua inaandaa mazingira mazuri kwa mbu kuzaliana.

Je serikali inafanya nini kutatua kero hii? Na wananchi wana mchango gani katika kutatua tatizo la mitaro kuziba na taka kutapakaa kila kona ya jiji la Dar es Salaam?
 
Mheshimiwa mvua iliyonyesha jana 29/09/08 ilileta msongamano wa magari barabarani. Kuna wengine walikua na magari vimeo yakaziomika yani tabu tupu. Waliokua kwenye daladala ndo usiseme.

Hivi wale wachina waliokua na mkataba wa kutengenezaq mitaqro pale kariakoo ilikuaje? mbona walichimba lakini bado maji yametwama.

Kero nyingine ni pale Waterfront building barabara ya Sokoine. pale kuna maji yamejaa. Cha kushangaza ile ndo njia ya Mhe. Raisi na wageni wake wakiwa wanaenda Airport wakitokea Statehouse.

Wahusika wako wapi?? au ndo mambo ya EPA.
 
Back
Top Bottom