Mvua imeleta maafa Chato na kusababisha vifo

Mvua imeleta maafa Chato na kusababisha vifo

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Chato. Mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji cha Mwekako kata ya Kasenga wilayani Chato mkoani Geita imesababisha vifo vya watoto wawili na kuharibu mali.

Diwani wa Kata ya Kasenga, Damian Vilarie amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema mvua imesababisha uharibufu wa miundombinu ya barabara.

Amesema mvua hiyo iliyonyesha kwa saa tatu jana Alhamisi Januari 11 ilisababisha mafuriko yaliyowasomba watoto wawili wa mzee Kurwa waliotoka soko la Igalula kununua bidhaa za nyumbani.

Amesema watoto hao mmoja anakadiriwa kuwa na miaka 13 na mdogo miaka mawili.

Chanzo: Mwananchi
 
Nami nawapatiliza wana maovu ya Baba zao....hata kizazi cha tatu na cha nne.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom