figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imeleta maafa makubwa katika kata ya Ikuti wilayani Rungwe, baada ya kuezua nyumba 23 na kuangusha migomba yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 250.
Mvua hiyo ambayo imenyesha kwa muda mfupi lakini ikasababisha madhara makubwa, imemlazimu mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, Abbas Kandoro, kutembelea eneo ambalo limeathiriwa na mvua hiyo ambapo amepokea taarifa ya uharibifu wa mali za wananchi kutoka kwa afisa kilimo wa wilaya ya Rungwe, Godwin Katiko.
Baada ya kusikiliza madhara ambayo yamesababishwa na mvua hiyo, mbunge wa Rungwe, Sauli Henry Amon akaguswa na tatizo la wananchi hao kukosa mahali pa kuabudia, kutokana na kanisa lao pia kuporomoka.
Akihitimisha ziara hiyo, mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akaagiza kuitishwa kwa kikao cha dharura cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe ili kujadili namna ya kuwasaidia wananchi hao, badala ya kusubiri msaada kutoka serikali kuu.
Chanzo: ITV