MV CCM...... Arusha kina kirefu!!!!!

MV CCM...... Arusha kina kirefu!!!!!

Uda

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Posts
811
Reaction score
623
Alianza makongoro kuwaletea kihoro
Nccr ya mrema ikatutia kilema
Fitina tukazisema eti pombe kilema
Mwisho wake mahakama mbunge akasimama
Chama mama bila hiyana mkazicheza na rafu
MV CCM……Arusha kina kirefu

Elfu mbili na tano ndani ya mji karatu
Dr willy akiwemo akawapiga matatu
Shuhuda ni
Molemo tukayaona mavitu
Halmashauri mfano kwa visima virefu
MV CCM….Arusha kina kirefu

Tukalicheza kandanda elfu mbili na kumi
Chini ya lema kamanda yumo lakini havumi
Dada mary chatanda kidogo kupigwa ngumi
Huku mizengo kapinda na porojo Tamisemi
Tuliohisi makamanda wakahongwa makumi
Vijana wakavurunda tukaikosa na safu
MV CCM ……Arusha kina kirefu

Mimi bado nawaza risasi za januari
Vipigo vilianza maandamano halali
Hata kama ni vilaza maisha ni halali
Sonono zikatulaza polisi kuleta shari
Meya feki katukwaza katuletea hatari
Kama kule mwanza mgogoro mrefu
MV CCM….Arusha kina kirefu

Alazwe pema peponi Mheshimiwa Sumari
Tukalinda kama mboni kura za nassari
Dogo janja bila soni akachora mstari
Kura zote shishtoni na hata kule kitefu
MV CCM….Arusha kina kirefu

Mkutano Soweto mkatupiga mabomu
Mkaua watoto mkatunyima salamu
Msibani mkongo'to yaani sina hamu
DVR zimeseto kugundua uchafu
MV CCM ….Arusha kina kirefu






Julai kumi nne siku hiyo jumapili
Mida ya saa nne dakika kumi mbili
Ni magoli manne kijani wako chali
Mwigulu na wengine wapata kichefu chefu
Makamanda Arusha twajimwaga Jey Efu
MV CCM,,,,,,Arusha kina kirefu

cc
Mungi LIVEPOOLfc Preta Jackbauer Rutashubanyuma Mzee Mwanakijiji Arushaone Filipo PakaJimmy Mingoi Ritz
 
hii ni zawadi kwa wana arusha wote,sina cha kuwapa wote mridhike lol!
 



Julai kumi nne siku hiyo jumapili
Mida ya saa nne dakika kumi mbili
Ni magoli manne kijani wako chali
Mwigulu na wengine wapata kichefu chefu
Makamanda Arusha twajimwaga Jey Efu
MV CCM,,,,,,Arusha kina kirefu



maneno swadakta haya.
kumeza ngumu kutema ngumu
 
Shori acha kujigamba
punguza huo ushamba
Namkumbuka makamba
zee la kisambaa
chama alikipamba
kama brazil kwa samba
mifedha tukailamba
kunenepa kama komba
tukaota na magamba
kama nyoka na mamba
leo hii tumelambwa
mchemba mwampamba
watorokea kibamba
kweli ccm imekifu
hiki kina kirefu

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Shori acha kujigamba
punguza huo ushamba
Namkumbuka makamba
zee la kisambaa
chama alikipamba
kama brazil kwa samba
mifedha tukailamba
kunenepa kama komba
tukaota na magamba
kama nyoka na mamba
leo hii tumelambwa
mchemba mwampamba
watorokea kibamba
kweli ccm imekifu
hiki kina kirefu

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

dah....kweli JF kiboko........nimeipenda......
Next malenga plz.......
 
Kijani aina rutuba pote pakavu, hawana sera mbele ya makamanda wa ukweliii!!!!!!
 
Nchemba jifanya Njemba,
Nahodha kinda shika sukani,
Ubabe jitia mjivuni mtu,
Hofu tawalisha kampeni.

Utisho tanguliza longlongo,
Kampeni za utisho giza kiza,
Utusitusi bananisha abongapo,
nguo watu chojoa hovyo.

Matusi mdomoni povu toka,
akili ndogo kihayawani,
Mwigulu shule karatasi DESSA,
Elimu siri sifuri.

MV CCM chombo selea,
Nahodha hofuni mcheche telu,
Mv CCM kilindini zama,
Nahodha Benzi atokomea.

Timu timu kilemba acha nyuma,
Bawa epusha woga tawala,
GreenGuard wajiju kilindini,
Mwigulu mitini naingia.

Lameki Nahodha Kinda duchu,
Ushindi lilia maziwa mama,
Lameki mjivuni u wapi,
Ziko wapi ngebe zako??

 
Shori acha kujigamba
punguza huo ushamba
Namkumbuka makamba
zee la kisambaa
chama alikipamba
kama brazil kwa samba
mifedha tukailamba
kunenepa kama komba
tukaota na magamba
kama nyoka na mamba
leo hii tumelambwa
mchemba mwampamba
watorokea kibamba
kweli ccm imekifu
hiki kina kirefu

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
JF kisima cha burudani, duh nimependa hapa zaidi ulivyomalizia.... ila umesahau Shoza pia alikuwa kibamba ndiyo kaibuka leo asubuhi.

tukaota na magamba
kama nyoka na mamba
leo hii tumelambwa
mchemba mwampamba
watorokea kibamba
kweli ccm imekifu
hiki kina kirefu


 
huu mtumbwi wa ccm una hali mbaya sana.
Umshakunywa maji mwanza,mtwara,mbeya na sasa arusha
Tunausubiri dar tuutoboe uzame kabisa
 

Julai kumi nne siku hiyo jumapili
Mida ya saa nne dakika kumi mbili
Ni magoli manne kijani wako chali
Mwigulu na wengine wapata kichefu chefu
Makamanda Arusha twajimwaga Jey Efu
MV CCM,,,,,,Arusha kina kirefu

cc
MungiLIVEPOOLfc PretaJackbauerRutashubanyumaMzee MwanakijijiArushaoneFilipoPakaJimmy MingoiRitz

Yote tisa, mambo yote ni elfu kumi na tano
Atakayeshinda Ikulu huyo kweli ndiye mbabe
Kura zikiibwa asiwepo wa kulialia tena hapo.
Mkakati wa kuzilinda kura hilo nalo sasa fumbo.
CDM kweli chenga yatula lakini mabao ni dakika 90.
Ushindi wa awali hauna zengwe kama utaishia papo.
 
Leo tena katamba kamanda Ally Bananga!
Sombetini si kibamba bao moja twawalamba!
Arusha si washamba hakika tumewabamba!
Niko hapa KWA MREFU na mabraza wa Cuf!
Mv ccm Arusha kina kirefu!
 
chadema ni burudani

baada ya kifinyo mmehamia kwenye ngonjera
 
Back
Top Bottom