Muziki Wetu Vipi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
219
“ Karibuni Kenya , Nchi ya jua , jambo jambo kaka jambo jambo rafiki , twende tukaone wanyama ,twende safari tukaone samba na wenzake wakilindaaa “

Hayo ni maneno yaliyo katika CD inayoitwa Best Afrikan Songs , nyimbo hizo zimeimbwa na bendi moja inayoitwa SAFARI SOUND BAND maskani yake nchini Kenya , wiki hii nilivyoenda katika rafiki yangu wa Kenya alinipatia CD hii kama ukumbusho .

Niliona aibu sana kwa sababu yeye alitaka na mimi nimpatie CD za huku au nikirudi nimtumie baadhi ya hizi nyimbo zinazoelezea baadhi ya mambo ya tanzania haswa mbuga za wanyama , hifadhi za taifa , milima mito na mabonde zote hizi sikuwa nazo .

Nilipooangalia tena hii CD nikaona namba 11 kuna nyimbo moja inayoitwa KILIMANJARO , Kilimanjaro mlima mrefu sana , Kilimanjaro unapendeza sana nikamwomba basi asikilize hiyo nyimbo ya Kilimanjaro kwa sababu uko nchini kwetu Tanzania .

Ubishi ukaanza pale rafiki yangu akanifungulia katika www.youtube.com akanionyesha nyimbo hiyo ya Karibuni Kenya Video yake , katika moja ya hizo picha unaonekana mlima Kilimanjaro na upo upande wa Kenya nikaamua kusalimu amri .

Ninachotaka kusema Serikali yetu pamoja na wadau wengine wanaohusika na masuala haya sasa waje na jitihada mpya za kutangaza vivutio vyao kwa njia mbali mbali kuanzia hiyo kutengeneza nyimbo za Kiswahili zinazosifia au kuelezea mambo ya Tanzania .

Mfano ukisikiliza hii cd ya Safari Sound kuna nyimbo kama Jambo Jambo , Pole pole , Nakupenda wewe , Music in Africa , Coconut , Kenya Safari ,Mombasa , Ahsante Sana na nyimbo zingine zinazoelezea Kenya kwa kina pale mtu anaposikiliza .

Ninapojaribu kutafuta duka ambalo naweza kukuta nyimbo za kusifia nchi yangu hata sipati hata sijui zinauzwa wapi .nyimbo zote unaweza kukuta zimetengenezwa na watu wan chi zingine .

Ukisikiliza nyimbo kama SERENGETI iliyoimbwa na Hugh Masekela wa afrika ya kusini tunaweza kutumia nyimbo kama hii kama kivutio katika hizi CD kuna nyingine inayoitwa Zanzibar nayo imeimbwa na mwanamuziki wa afrika ya kusini tunaeza kuunganisha katika Collection moja .Pia kuna nyimbo kama Afrika nyimbo hii imeimbwa na Bendi moja inayoitwa TOTO kuna marashi ya pemba iliyoibwa na Ndala Kasheba .

Kuna nyingine nyingi za kuitambulisha Nchi sehemu mbali mbali mbapo mtu anatembelea .

Nitamaliza kwa maneno haya

We must begin to stand up for Kenya. Kenya is bigger than any single tribe or leader. We must begin to teach our children to respect and love our country. We must stop the negative attitude about our beautiful country. Our diversity must become our strength. When it comes to Kenya, let us hang our tribal and religious labels and be Proudly Kenyan. When we are out and inside Kenya let us sell Kenya as a great brand. Great brands posses’ great attributes. Such great attributes must be communicated positively, both verbally and by our actions/behaviour. PROUDLY KENYAN!
A talk by Eric Kimani to the Final 2007 Nairobi Marketers Night on 7th December 2007


MCHANA MWEMA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom