Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,245
Muziki wa Tanzania, Asili ya utamaduni ni Tanzania
Inapotendeka ni Dar es Salaam
Lakini tuliimba, tulicheza ngoma, tulipiga vyombo mbalimbali, ila tulikuwa na utamaduni mwingine kuhusu kitu hiki tunachokiita siku hizi muziki. Watafiti wanatuambia tulikuwa na ngoma, ambayo tafsiri yake ni kubwa kuliko muziki.
Ngoma ilikuwa ni chombo kile kilichotoa muziki, ngoma ilikuwa shughuli yenyewe, kwa mfano ngoma ya mavuno, ngoma ya mashetani na kadhalika, na pia tulicheza ngoma. Pamoja na kukosekana kwa maandiko yenye kina kuhusu hali ya ngoma katika kipindi hicho lakini tunajua watu waliimba na kucheza ngoma kwa matukio mbalimbali, hali ambayo inaendelea mpaka leo.