Malcolmx Shabaaz
Senior Member
- Nov 21, 2017
- 128
- 174
MUZIKI NI HARAKATI
SEHEMU YA KWANZA: MIRIAM MAKEBA
Muziki ni sanaa; ni ufundi wa kuwasilisha mawazo yaliyomo katika fikra za binadamu kwa njia ya sauti na vyombo vya muziki ili kufikisha ujumbe kwa walengwa. Sanaa ya muziki hubeba ujumbe wa aina mbalimbali ikiwemo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Muziki huliwaza, muziki husaidia kurejesha afya kwa baadhi ya maradhi yatokanayo na msongo wa mawazo, muziki huelimisha, muziki hueneza fikra za ukombozi na muziki huhifadhi amali za jamii.
Tanzania na ulimwenguni muziki upo na ulikuwepo tangu enzi na enzi. Kwa leo nitauzungumzia muziki kama njia ya ukombozi. Ulimwenguni kote kulipokuwa na dhuluma muziki ulitumika kupigania haki za wanaodhulumiwa.
Amerika, watu weusi walionewa, walibaguliwa, waliteswa na waliuawa, mwisho, walitumia muziki kwa mfano Hip-hop kudai haki zao. Rege, pop, Afro-Jazz na aina zingine za muziki zimetumika kudai haki za watu wanaoonewa. Hata Afrika Kusini muziki ulitumiwa na watu kama kina Luck Dube kupigania haki za mtu mweusi.
Tuangazie macho yetu kwa Nguli wa Muziki, Mwanaharakati Miriam Makeba a.k.a Mama Afrika.
Miriam ni nani?
Mama huyu jasiri ana asili ya Afrika Kusini, alizaliwa mnamo tarehe 04 Machi 1932 huko Prospect, Johannesburg, Afrika Kusini. Mama yake alifahamika kwa jina la Christina Makeba mwenye asili ya kabila la Swazi na baba yake alifahamika kama Caswell Makeba ambaye alikuwa ni Xhosa kwa kabila.
Binti huyu alikumbana na mkasa wa kufiwa na baba yake mzazi akiwa bado yu mdogo sana na ndipo maisha yake yalipoanza kuyumba hasa katika elimu. Kipaji chake cha muziki kilidhihirika tangu yu mdogo jambo ambalo lilimfanya afungue ukurasa mpya wa sanaa.
Akiwa yu mdogo alijiunga na kundi la muziki liitwalo Cuban Brothers akiimba kwa kuiga nyimbo za Ki-Marekani jambo ambalo lilimfanya aanze kusikika kwa kiwango fulani. Alipofikisha umri wa miaka 21 alijiunga na kundi liitwalo Manhattan Brothers ambapo mwaka 1953 alifanikiwa kutoa nyimbo yake ya kwanza Laku Tshoni Ilanga iliyomtambulisha vema na kumuongezea umaarufu.
Aliendelea na muziki kwa kuimba na makundi mengine ikiwemo kundi la Skylarks lililoundwa na wanawake tupu. Makeba alijikita katika muziki wa ukombozi kwa staili ya Afro-pop, muziki wa kumkomboa mtu mweusi aliyekuwa akiishi kama mnyama.
Makeba kupitia muziki amefanya muziki maeneo mbali mbali ya ulimwengu huu ikiwemo Uingereza, Marekani na Italia. Akiwa Marekani alifanya muziki kwa ukaribu zaidi na Harry Belafonte, mwanamuziki Mmarekani.
Akiwa nchini Marekani, Makeba alizuiwa na serikali ya Makaburu kurejea nchini Afrika Kusini kwa sababu alikuwa mkosoaji mkuu wa wahalifu hao waliomnyanyasa na kumtesa mtu mweusi. Makeba alikumbana na mkasa mbaya sana mwaka 1960 baada ya tukio la mauaji ya Sharpeville kuteketeza ndugu zake wawili akiwemo mama yake mzazi, alipotaka kuja katika maziko, alizuiwa, hivyo kuamua kuishi Marekani rasmi.
Pamoja na kupokwa haki yake ya kurejea nchini kwake, Makeba alipata bahati ya kupewa uraia wa heshima katika nchi zipatazo kumi ikiwemo Ghana, Guinea na Ubelgiji. Maisha yake Marekani yaliingia mgogoro mara baada ya Makeba kuolewa na mwanaharakati mweusi nchini Marekani Stokely Carmichael mwaka 1968 hatimaye wawili hao kuamua kuondoka Marekani na kwenda kuishi nchini Guinea kwa Ahmed Sekou Toure!
Katika muziki, Makeba alifanikiwa sana kwa kufanya vizuri si Afrika tu bali ulimwenguni kote. Amefanya matamasha makubwa ya muziki Marekani, Italia, Ubelgiji, Ethiopia siku ya kuanzishwa kwa Umoja wa nchi huru za kiafrika, pia amewahi kushiriki onyesho maalum kwa Rais John Kennedy wa Marekani nk.
Makeba alikuwa mwanamuziki mwanaharakati; ameshiriki matukio makubwa ya kiuanaharakati ikiwemo tukio la kuanzishwa kwa O.A.U mwaka 1963 ambapo alishiriki kama mwimbaji huko Ethiopia.
Makeba alishiriki harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, mnamo mwaka 1955 alikutana uso kwa uso na mwanaharakati Nelson Mandela katika harakati za kumkataa kaburu! Makeba ameshiriki matukio kadhaa ya kupinga ubaguzi wa rangi ikiwemo tukio la filamu iliyofahamika kama Come Back, Africa.
Makeba ameshiriki harakati za ukombozi wa nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Kenya ambapo alikutana na Jomo Kenyatta mwaka 1962 na kuendesha harambee ya kuichangia Kenya fedha za kukamilisha harakati za ukombozi. Makeba alishiriki pia harakati za ukombozi wa Msumbiji iliyopata uhuru mwaka 1975 kutoka kwa Wareno, na mataifa mengine mengi Afrika.
Anakumbukwa pia katika ushiriki wake katika harakati za kumkomboa mtu mweusi Amerika dhidi ya ubaguzi wa rangi. Alishiriki kuyasaidia makundi mbali mbali ya haki za kiraia Marekani ikiwemo Black Power Movement, Black Panther Party na SNCC. Ameshirikiana na wanaharakati wakubwa Marekani kama Stokely Carmichael, Martine Luther King Jr, Malcolm X , Bobby Seale na wengineo wengi.
Makeba alirejea Afrika ya Kusini mwaka 1990 mara baada ya Makaburu kufungua milango kwa wafungwa waliokuwa uhamishoni na kuwaachilia huru waliokuwa gerezani kwa mfano Nelson Mandela. Alishiriki kukamilisha ukombozi wa nchi hiyo mpaka ilipopata uhuru kamili mwaka 1994 na kuongozwa na Mwafrika, Mzee Nelson Mandela!
Makeba anakumbukwa kwa nyimbo kadhaa za harakati ikiwemo A Luta Continua, Soweto Blues na zingine nyingi!
Mashairi ya Wimbo A Luta Continua (Mapambano yanaendelea).......
My people, my people open your eyes
And answer the call of the drum
Frelimo, frelimo,
Samora machel, samora machel has come.
Maputo, maputo home of the brave
Our nation will soon be as one.
Frelimo, frelimo,
Samora machel, samora machel has won.
Mozambique a luta continua
A luta continua, continua, continua. (4 times)
And to those who have given their lives,
Praises to thee
Husband and wives, all thy children
Shall reap what you sow
This continent is home.
My brothers and sisters stand up and sing,
Eduardo mondlane is not gone
Frelimo, flrelimo, your eternal flame
Has shown us the light of dawn,
Mozambique a luta continua
A luta continua, continua, continua
In Zimbabwe a luta continua
A luta continua, continua, continua
In Botswana a luta continua
A luta continua, continua, continua
In Zambia a luta continua
A luta continua, continua, continua
In Angola a luta continua
A luta continua, continua, continua
In Namibia a luta continua
A luta continua, continua, continua
In South africa a luta continua
A luta continua, continua, continua
FUNZO KUTOKA KWA MAKEBA: Si lazima muziki uimbwe kuhusu mapenzi na anasa za dunia wakati jamii imejaa matatizo tele, wasanii watumie muziki kuukomboa umma wa wanyonge na siyo kuwaza anasa tu muda wote!
Makeba aliaga dunia tarehe 09 Novemba 2008 nchini Italia. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, AMINA!