Muziki kutoka nchini Zaire (sasa ni D.R.C) uliwezaje kutamalaki na kupendwa sana hapa Tanzania ilhali tumepakana na jirani wengine takribani 6?

DRC, batoto ba Congo.......Mobutu ama (Kuku mbengu wa Zabanga), ni kweli alichukia sana mambo ya kuiga umangaribi, lakini hapo hapo akawa anatamani sana maisha ya Kifaransa!...baada ya kuwaambia bana ba congo kuacha majina ya kikoloni kama vile Franco ama Rochereau...ambao wakati huo ndio walikua wakali wa muziki, Majina ya kabakia Luambo Luanzo Makiadi na Tabu Ley.

Mobutu kapiga kampeini kubwa sana ya kuondoa Ukoloni mambo leo , ndio mpaka sasa Congo Drc kuna Dini na kanisa la ki itikadi ya Kiafrika inayoitwa 'Kimbangiste'..... Makanisa yalibaki kufunza vijana kupiga muziki.....vile vile kwa vile walitawaliwa na Wafransa, kuna kitu kinaitwa ''Assimilation" yaani kuigiza aliekuteka mpaka ufanane nae...ilibidi watafute vyombo na machine za kurecodi za hali ya juu sana, ndipo unaona ngoma zao nyingi ni kali mpaka kesho...rekoding either Paris , belgium ama Us!
Naam
 
Safi sana mkuu...
 
Swali zuri sana;

Utamaduni wa ndugu zetu wa kongo unaendana sana na Muziki pamoja na kucheza Muziki. Wakiwa wanalima watafanya hivyo iwapo kuna watumbuizaji wa muziki na hata kwenye mazishi huwa wana watumbuizaji wa muziki; na lolote wnalofanya kama jumuia lazima kuwe na muziki. Hii ni tofauti sana na kwetu huku ambako muziki ni burudani tu. Sasa wanamuziki wa Kongo waliamua kuchukua muziki wao kwa next level ili ujulikane ni muziki wa Kongo, na wakafanikiwa sana. Kwa hiyo muziki ni sehemu ya maisha yao na nyimbo nyingi unazojua za kikongo zina asiili muziki wa makabila yao. Tanzania na Uganda hatujawahi kuwa na muziki ambao ni brand ya Tanzania au ya Uganda, huwa tunakopi Kongo tu labda ukitoa ukitoa taarabu. Kenya walijaribu Benga kidogo lakini nadhani nao walifeli.
Wakenya hawajui kabisa music mkuu...
 
1. Walijua mapema kwamba muziki ni kazi na siyo starehe tu.
2. Walichanganya vionjo vya kongo na vile vyenye asili ya Cuba ambavyo zama hizo asili yake ilikuwa kongo basin
3. Walijenga mapema zaidi matumizi ya lugha yao kimuziki na kwa nguvu kubwa
4. Mabepari wa kigiriki walifungua "nyumba" za muziki na kuajiri session musicians kutoka DRC, Brazza, Angola etc na kujenga mashindano makali. Santuri zilitengenezwa na kuuzwa nje. Bendi zote kuu African Jazz, Rock A Mambo pamoja na OK Jazz etc zinahusika hapa.
5. Gitaa za umeme ziliingia mapema zaidi fuatilia midundo ya Orch. Watam na ilivyobadilika hadi OK Jazz miaka ya hamsini
6.Kuwa na wanamuziki wachache ambao walikuwa na ubunifu wa hali ya juu sana mmoja wapo akiwa Franco the Genius aliyejaribu kujiongeza kila idara, alihahakisha ngoma zake zinaendana na midundo ya kiafrica. African Jazz ilikuwa ya kisomi zaidi na OK Jazz ilikuwa ya mtaani. Kwa mfano OK Jazz na baadae TP OK Jazz ingawapo wengi wetu wanamjua Franco tu, lakini ilikuwa na nguzo kali kama Vicky Longomba (Baba yake Awilo) na huyu ndiye alikuwa sauti ya OK Jazz 1956-1971 na mtunzi mahiri (Co-president wa OK Jazz), Simaro Masiya Lutumba (1961-1993), Chef d'Orchestre, mpiga rythm mashuhuri, mtunzi bora wa OK Jazz na TP OK Jazz (The Poet),Vice President na President wa bendi baada ya Luambo kufariki na bila kumsahau Kiambukuta Londa Josky (1973-1993) mtungaji bora, muimbaji bora kabisa wa TP OK Jazz-kama Vicky alikua sauti ya OK Jazz basi Josky ndiye sauti ya TP OK Jazz (Comandant du Bord) alikuwa Vice President wa TP OK Jazz baada ya kufariki Luambo.
7. Nidhamu ya hali ya juu na mazoezi ya kufa mtu ili kutoa kitu kinachoeleweka.
8. Mobutu alisaidia lakini kikubwa zaidi ni wanamuziki wenyewe kujituma.
9. Bendi za DRC zilisafiri sana ndani na nje ya nchi na hivyo kueneza muziki wao
10.Baada ya wagiriki kuachana na muziki wazawa kama Verckys wa Maison Veve na Luambo waliingia sana kwenye biashara ya santuri na kufanya Kenya kwa Afrika mashariki kuwa kituo kikuu cha kutolea santuri zao (ASL) na hivyo kupatikana muziki wao wkwa urahisi zaidi.
11. Mpangilio wao wa mziki: mfano mzuri ni matumizi ya magitaa manne kwa wakati mmoja ambayo nafikiri ni Afican Jazz/Fiesta ndio walianza lakini Franco aliposhika hii kitu akaipaisha kwa namna ambayo haijatokea na kila gitaa likisikika kikamilifu na kwa kiwango bora zaidi na ndio maana haitarajiwi tena kutokea bendi kama TP OK Jazz.
12. Mwisho wa yote-hizo ni sababu zilizochangia wenzetu hao kuja na mirindimo bora ya kiafrica na kuisambaza kwa hamasa kubwa na kukubalika na waafrica wengi.
Ufafanuzi makini sana huu mkuu
 
Back
Top Bottom