Muweka hazina wa CCM, mbunge Iramba Magharibi akimbia maswali ya posho na katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muweka hazina wa CCM, mbunge Iramba Magharibi akimbia maswali ya posho na katiba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jogi, Jul 3, 2011.

 1. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  wanajamvi, leo jioni nimeshuhudia mbunge wa iramba magharibi ambaye pia ni muweka hazina wa ccm, Mwigulu madelu nchemba, akikimbia hoja za wapiga kura wake, awali akihutubia wananchi kata ya kyengege alilalamikia suala la vijana kujiunga na chadema kana kwamba haijawafanyia chochote kwacho waiunge mkono, akitumia misamiati ya kinyiramba yenye kejeli aliwaambi alikuwa tayari kuwapatia ngombe wachinje wale ili warudi ccm, kwa jinsi alivyokuwa akilalamika na yeye mwenyewe kukiri kuwa jitihada zake zimegonga mwamba. aidha Mwigulu alitumia muda mwingi kuhutubia badala ya kutoa nafasi iliyosubiriwa kwa hamu kubwa ya maswali kwa muwakilishi huyo, ni kijana mmoja tu aliyelazimisha na kupata nafasi kumtwanga swali lililohusu uwakilishi mbovu bungeni, akijibu swali hilo alidai ni kutokana na tabia ya wapinzani bungeni kupinga kila kitu hivyo akalazimika naye kupinga. kigongo cha swala la katiba mpya na posho akasema muda umekwisha kwani saa 6.00 jioni ilishawadia, wananchi hawakufurahishwa na hilo, wamesikika wakisema
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,128
  Trophy Points: 280
  safi sana. Magamba yananeemeka na posho wakati wananchi wanakufa njaa vijijini.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sijasikia ile kauli mbiu ya MLITUTUMA TUMETEKELEZA,sijui iliishia wapi?????
   
 4. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hilo la posho litawatoa jasho iwapo wapiga kura wataielewa vizuri hoja hyo.CCM ina hali ngumu!
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  anaweweseka kwa taarifa kuwa dr Wilbrod Slaa atafanya ziara ya kuimarisha chama pamoja na maeneo mengine, pia kata ya kyengege, amejaribu kutumia maneno na misamiati mingi kuwarubuni wananchi wasihudhurie, jambo lilopingwa na vijana waziwazi.
   
 6. z

  zamlock JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  huyu mbunge si ndiye alikuja hapa tegeta na akafanya mkutano wakutaka kuwapa vijana msaada wa pikipiki eti waiunge ccm mkono na raisi kikwete ndiye atakayekuja kuzindua mradi huo wa kugawa pikipiki na tulipomtaka atueleze ni kwa nini aje hapa kutaka kutoa msaada wa kugawa pikipiki kwenye hili jimbo la kawe na badala ya kwenda kwenye jimbo lake atoe msaada huo ndipo alipokosa majibu na kusemekana kuwa mpango wake huo nikutaka kuja kugombea ubunge jimbo la kawe hakiki alikosa majibu na akakimbia na wenzake aliokuwa amekuja nao
   
 7. Mmang'ati

  Mmang'ati Senior Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 185
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Namfahamu huyo jamaa tangu Mazengo complex(sec)alikuwa vice hp then akamfanyia hp fitna mpaka jamaa akarisign ye akawa hp. Zake ni fitna,rushwa na ujivuni c m2 mzuri hata chembe.
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  nakuunga mkono, alijisifu kuwa yeye ni mchumi first class, yeye amebahatika kuitwa na kuongea na kikwete, yeye amefika ikulu. unaweza kukosea badala kucheka ukaanza kulia!!!!
   
 9. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Bwana mdogo makamasi yanamsumbua
   
 10. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Singida ni mojawapo ya maeneo masikini kabisa ktk nchi yetu,kama wamechagua mbunge ambaye kazi yake ni kusifia serikali badala ya kuibana ipeleke maendeleo basi imekula kwao! Naomba wana JF mnaomfahamu vizuri huyo jamaa mtuhabarishe zaidi. Hii tabia ya wabunge wengi wa CCM toka maeneo masikini kusimama bungeni na kusema wanaunga mkono asilimia mia kwa mia bajeti ama miswaada ya serikali hata kama haina manufaa kwa wananchi wao,inazidi kuongezeka. Siku hizi siwasikii wabunge wa Mtwara, Lindi, Pwani nk wakitoa hoja nzito bungeni na kuibana serikali ili ipeleke miradi ya maendeleo ktk mikoa yao ambayo ipo nyuma sana kimaendeleo.
   
 11. k

  kings09 Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kweli majimbo ambayo yapo nyuma ki-maendeleo ndio mtaji kubwa wa kwa ccm, tazama singida yote, dodoma yote, wao bado wanashangilia kupata naibu wa spika bungeni wala hawana haja na maendeleo, tazama igunga, tabora yote, mtwara yote , lindi yote, tanga yote, ni maeneo ambayo kwa kweli yapo nyuma ki maendeleo.

  Bila kukuchosha, mwana JF, kuna wabunge huko bungeni wala hawajui kuwa wana muwakilisha nani?? kati ya chama au wananchi, kuna mbunge mmoja yeye ni mganga wa kienyeji, kutoka tanga, alisimama nakuanza kujisifia tuuuu, eti yeye ni maarufu kuliko wabunge wote wa uinzani, na tena yeye ametembea sehemu nyingi tu duniani kwa hio wabunge wa upinzani hawana hoja ya kumweleza yeye katembea sana na ni maarufu sana, basi hicho ndicho alichotumwa na wapiga kura wake nao wanafurahia.

  Mwingine alishawahi kuwa mtangazaji maarufu wa radio, nae alikuwa hana hoja ya msingi zaidi ya kuunga mkono hoja, na chakushangaza zaidi yeye pia alisimama nakuanza kusema kuwa ametembea nchi nyingi sana duaniani, nafikiri akipelekwa na radio kutangaza mipira, sasa anajisifia kuwa katembea nchi nyingi duniani ambazo ni maskini sana kuliko Tanzania,

  Sasa hoja yangu kwake kuna uhalali gani wa nchi hizo kufananishwa na nchi yetu, huwezi kufananisha nchi yetu na nchi kama Afrika ya kati, Chad, South Sudan, Burkinafaso, Mali, Congo Brazaville, Burundi, Rwanda, Zambia, Sierra Leone, Liberia, Guinea zote, na hata Kenya.
  Kikubwa sisi tuna raslimali ambazo hazitumiki vizuri ndio maana masikini, raslimali zingetumika vizuri tungekuwa kama, South Afrika, Rwanda ya leo, Botswana, Egypt, Tunisia, Angola ya leo Nigeria, Ghana, hizo kwa uchache.
  Wabunge kama hawa hawafai kabisa kuwa wawakilishi wa watu bungeni.
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  nimemuangalia cleopa david msuya, amesema jambo muhimu ambalo ndg. mwigulu hajui kulifanya, kupita na kuhonga honga wapiga kura. badala ya kuibana serikali ipeleke miradi ya maendeleo jimboni, anatoa fedha na vifaa bila maelezo ni kutoka fungu lipi (bajeti gani mshahara wake, posho au kutoka kwa wahisani) kwa sababu kama hazijulikani zatoka wapi, twaweza letewa fedha za kifisadi nasi tukashangilia kama mazuzu.
   
 13. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  ndiye mkuu, tena inasemekana alifanya mkutano na viongozi wa dini usiku jmosi kanisani, tunashawishika kuamini walikutana kwani wakati wakihutubu karibu wachungaji wote walisema ndg. mwigulu ni chaguo la mungu, hawakusema hivyo viongozi wa kidini wawili, mwinjilist mmoja na sheikh ambao walisema wao humuomba mungu kwa ajili ya viongozi wote akiwemo ndg. mbunge
   
Loading...