Huyu jamaa anawanyanyasa sana wafanyakazi, alileta tangazo humu mwaka uliopita mm nilikuwa na ndugu yangu nikamwambia aende, lakini alimnyanyasa sana, yeye ni muislamu, na mdogo huyo wa kike ni mkristo, yaani mdogo wangu alikuwa anafanyakazi masaa 12, Siku saba za wiki, hamna hata siku moja ya kumpuzika, mshahara 100,000! Mpaka mdogo wangu hakumaliza hata mwezi, na kuna mambo mengi sana pia ambayo alinieleza, maana huyo mdogo wangu kaenda huko Majirani wanamwambia huyo boss hakaagi na mfanyakazi!!
Jamani tulio na wafanyakazi tusiwanyanyase basi tuwachukulie kama wadogo zetu!!! Mpaka chakula mnamtenga mwenzio, ni jambo la aibu sana, haya mambo nayasikia uarabuni huko, lakini mpaka huku bongo huwezi aamini mambo haya yapo!!!