Muundo wa ligi kuu ya Tanzania ubadilishwe

wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
3,984
4,131
Kwa kuutazama huu muondo wa sasa hauleti ushindani na una mianya mingi sana ya hizi timu kongwe kuendelea kutawala.

Ingependeza baada ya mzunguko kuisha, ichezwe ligi ndogo walau ya timu sita tu ili kumpata bingwa wa ligi kuu ya Tanzania.

Zile timu sita za juu ndizo ziingie kwenye ligi ndogo ambayo itapigwa kwa mechi moja. (Sio home & away).

Hapa TFF wanaweza chagua viwanja bora kabisa ndipo baadhi ya mechi zipiwe huko.

Mfano wa viwanja ni Kaitaba, Lupaso,uhuru na chamazi.

Hii itaongeza ushindani zaidi lakini pia kushuhudia mechi zenye mvuto kwa mashabiki na kupata timu bora.

Hii itasaidia pia hata kwa marefa kutokuwa na presha, wala misheni town za timu kuunda matokeo.

Watasubiria kiumane kwenye hatua ya fainali ya hizo timu sita.

Pia hata kwa azam media itakuwa na tija zaidi,achilia mbali mapato ya viingilio.

TFF naomba ibadiri mfumo huu wa sasa wa ligi.

Alamsiki Bin Nuruuuu.
 
Kwa kuutazama huu muondo wa sasa hauleti ushindani na una mianya mingi sana ya hizi timu kongwe kuendelea...
Hizo timu sita za juu zitahamia kwenye ligi ndogo na ponits zake zile zile au wataanza upya?

Hii ya kuendelea na points zake nishaiona sana nje.
 
Hizo timu sita za juu zitahamia kwenye ligi ndogo na ponits zake zile zile au wataanza upya? Hii ya kuendelea na points zake nishaiona sana nje.
Mnaanza bila point.

Ukisema wahame na point,chukulie leo azam ameachwa point zaidi ya 20 na yanga. Haileti tija.

Wote wanaanza upya.
 
Kwa kuutazama huu muondo wa sasa hauleti ushindani na una mianya mingi sana ya hizi timu kongwe kuendelea kutawala...
Mleta mada ushauri wako uko too complicated&useless, sioni tija yoyote ikiwa ushauri wako utachukuliwa. Pia sababu zako zina mapungufu yafuatayo;

1. Huo mfumo ulioshauri hauongezi ushindani wowote, tena utaua ushindani. (Yaani timu iliyoshika nafasi ya sita kwenye ligi ikiwa imeachwa zaidi ya points 20 inaweza kutwaa ubingwa)

2. Utazidisha rushwa au upendeleo wa waamuzi (maana bingwa atapatikana kwa kushinda mechi moja kwa moja kwenye ligi ndogo ya timu sita tu)

3. Kuna klabu zitakosa mapato na mashabiki (Embu waza tu, timu za Dodoma Jiji na Mbeya City ikiwa zitaingia kwenye ligi ya sita bora, halafu mechi zao zote zichezwe nje ya viwanja vyao wanavyovitumia siku zote, nani ataingia uwanjani?)
 
Mbona Ubelgiji Wana huo mfumo na ligi Yao imetoa wachezaji wengi nyota duniani

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Mnaanza bila point.

Ukisema wahame na point,chukulie leo azam ameachwa point zaidi ya 20 na yanga. Haileti tija.

Wote wanaanza upya.
Napo pia haina tija,

Fikiria Yanga amemzidi Azam kwenye ligi ndefu aje akosee step kwenye mechi 5 tu za ligi ndogo kisha asiwe bingwa.

Yaan mfano ligi ndefu amzidi Azam points 20. Ligi ndogo aje azidiwe na Azam point 1 kisha Azam ndo awe bingwa, inakuja hii kweli?
 
Napo pia haina tija,
Fikiria Yanga amemzidi Azam kwenye ligi ndefu aje akosee step kwenye mechi 5 tu za ligi ndogo kisha asiwe bingwa...
Malizia alafu ndio akaiwakilishe nchi kimataifa yani mnacheza ligi badae timu 6 yupo Geita gold na Namungo.

Wanakukomalia mechi 1 wanapita halafu Geita gold anaenda Championship kuwakiliaha nchi
 
Malizia alafu ndio akaiwakilishe nchi kimataifa yani mnacheza ligi badae timu 6 yupo Geita gold na Namungo, wanakukomalia mechi 1 wanapita alafu Geita gold anaenda Championship kuwakiliaha nchi
Si ndo hapo,
Wakati ligi ndefu ulimpita zaidi ya points 30
 
Wanaanziaga points 0 kama alivyoshauri mleta mada?
Hapana, wa kwanza anaendelea kuwa wa kwanza mpaka wa 6. Zile point zinagawanywa kwa 2, sijajua lengo lao halisi, huwa nafikiri ni kupunguza gape la point ili msisimko uwepo, Hivyo mwenye point 60 atakuwa na 30,mwenye 50 atakuwa na 25 kisha mwenye 48 atakuwa na 24
 
Mwenye Points 41 je?
😀😀😀
 
Napo pia haina tija,

Fikiria Yanga amemzidi Azam kwenye ligi ndefu aje akosee step kwenye mechi 5 tu za ligi ndogo kisha asiwe bingwa.

Yaan mfano ligi ndefu amzidi Azam points 20. Ligi ndogo aje azidiwe na Azam point 1 kisha Azam ndo awe bingwa, inakuja hii kweli?
Kumzidi mtu point nyingi katika mechi nyingi kwa nchi kama yetu hakukufanyi uwe bora tukuamini.

Kama ubora unao utashinda hata hizo mechi chache

Ili ukirnda kimataifa ambapo ambapo nipo kuna kukamiana utakuwa umeiva.

Kuchezwa kwa ligi ndogo kutaleta ufanisi wa juu sana kwa vilabu na waamuzi.

Hata janja janja itapungua.
 
Back
Top Bottom