Muundo wa Elimu ya Tanzania

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Elimu nchini Tanzania hutolewa na sekta zote mbili, yaani, sekta za serikali na binafsi. Muundo wake kiujumla ni kama ifuatavyo:[

👉Miaka 2 au 1 elimu ya vidudu/cheke-chea hutolewa kwa wanafunzi wenye umri kati ya miaka 5–6 (miaka 2), lakini hii watoto sehemu kubwa wanaanza wakiwa na umri wa miaka 3, ili kuwa na mazoea ya shule.

👉Miaka 7 elimu ya msingi ambayo hutolewa kwa watoto walio na umri wa miaka 7–13 (Darasa la I-VII)

👉Miaka 4 elimu ya sekondari hutolewa kati ya umri wa miaka 14–17 (Fomu 1-4)

👉Miaka 2 elimu ya juu ya sekondari hutolewa kati ya umri wa miaka 18–19 (Fom 5 na 6)

👉Miaka 3 zaidi elimu ya Chuo Kikuu.
👉Pia Elimu ya Juu inaweza endelea zaidi Kama ifuatavyo.
Kwa kuanza na ngazi ya;
1-Astashahada/cheti(Certificate) kwa Mwaka mmoja.
2-Stashahada(Diploma) kwa Miaka miwili.
3-Shahada ya kwanza/Awali(bachelor degree/First degree) kwa Miaka mitatu(Baadhi ya kozi huchukua Miaka 3,4 au 5)
Note: hii Ni muundo wa Elimu ya Juu ulio onyeshwa hapo juu ambapo mtu husoma akimaliza elimu ya Sekondari ya Juu au mafunzo ya ngazi flani.
4-shahada ya uzamili/umahiri(Masters degree) kwa Miaka miwili.
5-shahada ya uzamivu/falsafa ya udaktari (Philosophy doctor)phd kwa Miaka 3,4,5,6 au 7.

Baada ya hapo hufata tafiti ambazo zinaweza kusaidia kupata sifa flani ya Elimu Kama vile associate professor na professor(full professor).

Hiyo Ni kwaufupi kuhusu Elimu ya Tanzania.

Imeandaliwa na Emmanuel Kasomi
 
Huo ni muundo wa kuchuja wanafunzi kupata wa ngazi inayofuata. Mfumo wa kizamani. Sera ya Elimu 2014 imeweka vizuri mfumo wa kulinganisha elimu (National Qualifications Framework, NQF). Ikitekelezwa vema, itafanya mageuzi makubwa.
 
Ukimaliza kusoma iyo miaka unakua umebakiza miaka 12 ustaafu 😂
 
Elimu nchini Tanzania hutolewa na sekta zote mbili, yaani, sekta za serikali na binafsi. Muundo wake kiujumla ni kama ifuatavyo:[

Miaka 2 au 1 elimu ya vidudu/cheke-chea hutolewa kwa wanafunzi wenye umri kati ya miaka 5–6 (miaka 2), lakini hii watoto sehemu kubwa wanaanza wakiwa na umri wa miaka 3, ili kuwa na mazoea ya shule.

Miaka 7 elimu ya msingi ambayo hutolewa kwa watoto walio na umri wa miaka 7–13 (Darasa la I-VII)

Miaka 4 elimu ya sekondari hutolewa kati ya umri wa miaka 14–17 (Fomu 1-4)

Miaka 2 elimu ya juu ya sekondari hutolewa kati ya umri wa miaka 18–19 (Fom 5 na 6)

Miaka 3 zaidi elimu ya Chuo Kikuu.
Pia Elimu ya Juu inaweza endelea zaidi Kama ifuatavyo.
Kwa kuanza na ngazi ya;
1-Astashahada/cheti(Certificate) kwa Mwaka mmoja.
2-Stashahada(Diploma) kwa Miaka miwili.
3-Shahada ya kwanza/Awali(bachelor degree/First degree) kwa Miaka mitatu(Baadhi ya kozi huchukua Miaka 3,4 au 5)
Note: hii Ni muundo wa Elimu ya Juu ulio onyeshwa hapo juu ambapo mtu husoma akimaliza elimu ya Sekondari ya Juu au mafunzo ya ngazi flani.
4-shahada ya uzamili/umahiri(Masters degree) kwa Miaka miwili.
5-shahada ya uzamivu/falsafa ya udaktari (Philosophy doctor)phd kwa Miaka 3,4,5,6 au 7.

Baada ya hapo hufata tafiti ambazo zinaweza kusaidia kupata sifa flani ya Elimu Kama vile associate professor na professor(full professor).

Hiyo Ni kwaufupi kuhusu Elimu ya Tanzania.

Imeandaliwa na Emmanuel Kasomi

Imeandaliwa na Emmanuel Kasomi - Siku nyingine weka references ya haya uliyoandika la sivyo utaonekana kama haya mavitu umetoa kichwani mwako.
 
Back
Top Bottom