Muulize Makonda leo, je, Gwajima ni muuza Dawa za Kulevya kama alivyomlaza mahabusu jana?

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,553
LEO HUSUTA

HAYA maisha yamesheheni sana unaridhawa. Je, sikukwambia?

Life is so wonderful, didn't I tell you? Leo inapofika, inaweza kukushangaza kuhusu jana. Leo hupatanisha maadui wa jana. Hufarakanisha marafiki wa jana. Leo huwafanya waja watamke kuwa ya jana ilikuwa kazi ya Shetani.

Mmh! Leo husuta na kusimanga. Leo hunyenyekeza. Zingatia hata leo itakuwa jana pale kesho itakapoitwa leo. Kuwa makini mwana!

Siku zote ishi kwa tahadhari ya kesho. Tambua kuwa kesho si tatizo la leo, isipokuwa pale hiyo kesho itakapogeuka leo. Halafu ya leo yakatamkwa ni ya jana.

Nawaona Kadinali Polycarp Pengo, Paul Makonda na Josephat Gwajima.

Muulize Makonda leo, je, Gwajima ni muuza dawa za kulevya kama alivyomlaza mahabusu jana?

Mtwange swali Gwajima leo, je, Makonda alighushi cheti cha kidato cha nne na jina lake ni Daud Albert Bashite kama alivyomtangaza jana?

Mhoji Gwajima leo, je, Kadinali Pengo ni mzee asiye na maana, aliyezeeka vibaya na asiyejulikana alikula maharage ya wapi kama alivyomshambulia jana?

Nimeshakwambia; jana inapogeuka leo, basi leo husuta watu, huwaumbua, huwalazimisha kuomba msamaha na kumsingizia mno Shetani.

Anyways, wazee walioniita mjukuu walisema tugange yajayo. Na yajayo ni matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020. Hasa Jimbo la Kawe. Gwajima anabeba matumaini ya CCM. Makonda pia ni mwana-CCM. Makonda na Gwajima wanachangia masilahi kwenye uchaguzi huu.

Umesahau mara hii? Nilikwambia Makonda atampigia debe Gwajima ili ashinde ubunge Kawe dhidi ya Halima Mdee wa Chadema.

This life is indeed wonderful. I told you!

Ndimi Luqman MALOTO
FB_IMG_1600883236072.jpg
 
Nami naunga mkono kuwa leo husuta. Fikiria Lissu alivyotoa mapovu kuwa Tanzania tutashtakiwa MIGA kwa kuwafukuza ACACIA. Leo hii ukilizungumzia hili wafuasi wake kama akina Tindo na Mmawia wanatoa povu kuliko Lissu mwenyewe!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom