eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,355
- 16,401
Shari inatafutwa bila sababu kwa sababu ya mwingine kujifanya mbabe kupitiliza zaidi ya wengine huku akujua kabisa ni kinyume na sheria za vyama
Wakat mwingine machozi yananitoka pale ninapoona kauli ya mtu ikiwa sheria na sheria ikiwa takatakaJPM anajua sana kwamba anachofanya ni kuvunja sheria waziwazi.. Lakini anafanya hivyo kwa sababu ameshaamua neno lake ndio liwe sheria hakuna zaidi ya hapo. Anayo majeshi na vyombo vingine vya usalama, yeye ndiye amiri jeshi mkuu atatoa amri na itatekelezwa. Ndio maana kasema anasubiri hayo maandamano halafu mtaona cha mtemakuni. Na mtu asidhani kwamba JPM anatisha tu, hapana atafanya kweli, kauli zake zinaonesha rangi yake halisi kwa waliokuwa hawamjui. Mara kwa mara akiongea utasikia nawaombeni tumtangulize Mungu katika kazi zetu. Lakini yeye mwenyewe hamtangulizi huyo mungu wake. Anaimba kama malaika anacheza kama shetani.
Mpaka sasa hivi hakuna mkutano wiwote wa vyama vya upinzani ambao umefanyika tangu JPM aingie madarakani na ukawa na hizo fujo, vurugu au uchochezi. Sasa ni kigezo gani kinatumika kuzuia! Anapiga ramli? Sheria zipo za kuwashughulikia waleta vurugu na fujo, kwa nini zisitumike endapo itatokea? Na kazi ya hao walinzi wetu ndio hiyo ya kuwashughulikia watu kama hao. Kuna jambo gani linaogopwa? Kukosolewa? Kupingwa? Hapana, nadhani kuna jambo limejificha. Muda utatoa jibu.
Wazee wetu walikufa wakitetea uhuru wa nchi yetu kutoka kwa wakoloniNgoja nikae pembeni nione hili timbwili linaenda vipi ila nikiangalia upande wa pili huyu mkuu wa kaya kama vile hatanii anaweza hata kutumia jwtz kutudhihirisha anachotamka na watu wakaambulia vilema vya kudumu pengine vifo cha msingi hawa wanasiasa wakae meza moja wapatane kikinuka wengine hatuna pakwenda ni tz na sisi sisi tz kwa hiyo watawala msituvuruge wananchi wenu tendeni haki kwa kira raia
hakika hatafika huko, hawezi kudumu miaka 10Kama hii ya vyama vya siasa anavunja nadhani hata ile ya ukomo wa madaraka itavunjwa tu