Muswada wa Katiba Mpya Kutua Bungeni April 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa Katiba Mpya Kutua Bungeni April 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Feb 23, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Muswada wa Katiba mpya kutua Bungeni Aprili

  Dodoma,8 February 2011

  SERIKALI katika kudhihirisha azma yake ya kuitikia mwito wa wananchi wa kuundwa kwa Katiba mpya, imetangaza kuwa itawasilisha bungeni, Muswada wa kuundwa kwa Tume itakayoratibu mchakato wa Katiba hiyo katika mkutano wa Tatu wa Bunge la 10, Aprili mwaka huu.

  Akisoma Tamko la Serikali bungeni, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema hatua hiyo inatokana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete katika salamu za mwaka mpya kwa wananchi, Desemba 31, mwaka jana akiahidi kuitazama upya Katiba ili iendane na miaka 50 ya Uhuru.

  Waziri Mkuu aliliambia Bunge kwamba, pamoja na kauli hiyo, Rais Kikwete alitoa kauli nyingine ya kusisitiza nia ya Serikali kuanza mchakato wa kuitazama upya Katiba ili kuunda mpya, Februari 5 alipohutubia kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa CCM, mjini Dodoma.

  Rais aliahidi kuunda Tume itakayohusisha pande zote za Muungano, lakini pia wanasiasa, wanasheria, wafanyabiashara, wanataaluma na wananchi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii ili kuratibu mchakato huo wa kuitazama upya Katiba.

  "Muswada utakaowasilishwa bungeni ili kujadiliwa, utahusu majukumu ya Tume, utaratibu utakaotumika kuendesha mchakato wa kupata maoni ya wananchi, namna ya kupata wajumbe wa Tume, kazi ya Tume na masuala mengine ya msingi," alisema.

  Alisema, hata bila shinikizo kutoka vyama vya CUF na CHADEMA, Serikali ilikuwa na azma ya kuitazama upya Katiba ili kuifanyia mabadiliko iweze kuendana na umri wa miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, kwa lengo la kustawisha maisha ya wananchi.

  Alisema ni kutokana na nia hiyo, ndiyo maana Serikali imekuwa ikiunda tume mbalimbali kuitazama upya Katiba kama ile ya Jaji Francis Nyalali ya mwaka 1991 na ya Jaji Kisanga ya mwaka 1998 kupitia White Paper.

  "Nia ya Serikali ni kuona inatazama upya Katiba ili kuwa na Katiba itakayowapeleka Watanzania miaka 50 ya Uhuru kwa mafanikio zaidi, kuliko kuendelea kuwa na Katiba ya sasa ambayo ilipatikana tangu wakati nchi yetu inapata Uhuru kutoka kwa Mwingereza," alisema.

  Tamko la Serikali limekuja siku moja tu baada ya Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, juzi kuweka wazi kuwa Bunge halitajadili hoja binafsi zilizotarajiwa kuwasilishwa na baadhi ya wabunge kuhusu kuundwa kwa Katiba mpya ya Tanzania.

  Katibu wa Bunge alisema hatua hiyo inatokana na kwanza, suala hilo kukiuka Katiba ya sasa na pili utayari wa Serikali kuanza mchakato wa kuitazama Katiba ili kuja na Katiba mpya, kwa kuzingatia kauli za Rais Kikwete.

  Source:The United Republic Of Tanzania -Prime Minister's Office |News |Muswada wa Katiba mpya kutua Bungeni Aprili

  My position:
  I support the move. But! Muswada huo ni lazima upitiwe na wadau mapema kabisa na wadau wahakikishe maoni na michango yao imefanyiwa kazi kabla ya kuwasilishwa kwenye bunge. Kwa kawaida serikali huchelewesha miswada tata hadi kikao cha bunge kikishakaa ndipo wanaita wadau kisha wanaomba radhi kwa sababu ya muda maoni yote hayataweza kufanyiwa kazi!!!
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Safi ila kuna jambo moja haipaswi kuwa kazi ya rais kuunda hiyo kamati bali kazi ya bunge. Tutadanganywa tu hapa, ingawa bunge hili nalo ni kama butu tu!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kwamba hata huyu mtoto wa mkulima tuliyemuamini sana naye kajiingiza kwenye kiswahili cha Pwani na kulizungushazungusha, mara hiki mara kile bila kueleka kitu, utadhani naye anataka kuimba taarab.

  Kubwa zaidi tunasubiri kuona kwenye mwada huo kama kweli wananchi tulielewana na kuchukua hatua kuandaa muswada wa wananchi au muswada wa CCM na viongozi wake.

  Hili tunalisubiri kwa sana kulidadavua. Kamwe harufu ya kuandaliwa katiba mpya kupitia sijui akina Bomani mara sijui Shivji haitovumilika; udalali hapa si ruksa hivyo muswada lazima uzingatie hilo na kuhakikisha kwamba uchaguzi ujao unafanyika chini ya katiba mpya na tume huru yauchaguzi bila visingizio zaidi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...