Mustakabali wa Watoto wetu uko shakani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,781
Nina hofu kuu kila nikitafakari na kuyaangalia mambo yanavyokwenda. Nawaangalia wanangu kisha roho inaniuma sana! Naona wazi kabisa napaswa, nahitajika kufanya jambo. Jambo kubwa kwa ajili ya kesho njema ya wanangu na wanao pia. Mimi nawe, sio wao na wana wao!

Tunaundiwa tabaka la watawala. Wao na wana wao, wajukuu na vitukuu, vilembwe na vining'ina! Kwamba akitoka mimi ni wewe halafu ni yule na yule walio kati yetu. Hakuna nje ya tabaka lao atakayeruhusiwa naye kuwa fulani kati yao!

Tunaundiwa tabaka la kimfumo, hesabu zao ziko kamili japo kwa kificho na kuzuga kwingi, wanachongeana njia na vichochoro, wanapeana connection, wanaundiana mitandao, wanachaguana, wanateuana, wanabadilishana na kupeana nafasi. Kama wewe si mmoja wao hupaswi hata kuwaza utapata lini kwenye nini na nini.

Tunaundiwa tabaka la elimu. Elimu ni ufunguo wa maarifa na uwezo wa kufanya maamuzi.. Wamejitenga na mfumo wetu wa elimu unaofubaza bongo za wanetu. Kamwe hawawezi kukubali wanao wapate maarifa sawa na wana wao,. Elimu ni silaha kubwa kwenye kudai haki ama kutengeneza mfumo! Wa kwao wanasomeshwa shule bora na vyuo bora.. Wanaandaliwa!

Tunaundiwa tabaka la kipato.. Kipato ni silaha pia ya kupambana panapohitaji maamuzi na matumizi ya nguvu.. Kwamba utake usitake lazima hili liwe. Ukikomaa sana kuna mawili wakumalize ama wakulambishe ukae kimya! Hapa kila mmoja kwa nafasi yake anajitahidi kukusanya nyingi awezavyo.. Nyingi nyingi zaidi nyingi kabisa.. Wanatambua nguvu ya shekeli penye udhia

Tunaundiwa tabaka la kijamii, kuna kwao na kuna kwetu, kwao kunatamanisha na kuvutia. Kwao kuna kila kitu katika mpangilio wake, katika utaratibu wake.. Je kwako hapo kwenu pakoje!? Kamwe hawawezi kukubali kwao pawe kwako na kwenyu pawe kwao.. Hawako tayari kufanya huo ujinga! Huduma za afya, huduma za msingi kuna tofauti kubwa kati yao na yetu

Tunaundiwa tabaka vijakazi wavuja jasho. Wakamuliwaji, wao ndio wakusanyaji na wapangaji..hawana huruma nawe. Wanachojali ni kukukamua mpaka tone la mwisho! Hawana huruma nawe, hawana mustakabali nawe, wanachojali ni wapate hata kile kidogo ulichobakiwa nacho. Hawa ni chui kwenye ngozi ya kondoo.. Utawekewa kila aina ya kodi na kila aina ya tozo! Wewe ni punda. SEMA MIMI NI PUNDA!

Tunaundiwa tabaka la waoga na wenye hofu, wepesi wa kusahau na wepesi wa kusifu na kuabudu... Tunaundiwa utii kwa shuruti.. Hutakiwi kusema LA bali hewala mkuu...! Ukienda kinyume ama ukahoji majina yote mabaya utapewa wewe.. Na ukijitia kushupaza shingo wana mkono wa ken vice kukunyorosha! Mwishowe ni woga , hofu na taharuki kila kona..!

Tunaundiwa taifa la vijana wa hovyo hovyo, wajinga wajinga wapuuzi puuzi. Wasio na maono, wasio na tafakuri, wasio na hekima, wasio na elimu, wasio na maarifa wala mustakabali. Wanachojua ni uchawa, umbea majungu na mambo mepesi mavazi na starehe huku wakiota ndoto za Alinacha na kusimuliana hekaya za Abunuwasi. Hakuna ubunifu bali kuiga na kunakili

Wanakushughulisheni na haya yote ili msahau yote yenye tija na yenye kubeba mustakabali wa kesho ya wanao. Vimeondoka vingi tulivyobarikiwa na Mola wetu. Walisaidia na kusaidiana kubeba vyote vinavyobebeka, vyote vimepigwa mnada kwa vipande vya fedha kidogo na ahadi ya madaraka. Wametengewa mafungu yao, wanakula mpaka wanavimbiwa.

Sasa ni muda wa kuanza kuchukua na visivyohamishika! Na wakivitaka watavichukua tu utake usitake. Nachelea kuwaona wanangu na vizalia vyao wakiwa watumwa kwenye ardhi yao wenyewe! Inaumiza sana! Kwakuwa wameshajijengea miisho yao itakayokoma vizazi na vizazi. Kazi ipo kwenye vizalia vyako na vyangu.

Kama umenielewa zinduka sasa. Tukaukomboe wakati kwa manufaa ya wana na wana wa wana wetu. VIZALIA HURU!
View attachment 2271736
 
Na visivyohamishika navyo vimefikwa bei
20220621_235422.jpg
 
Very Well Said !!! A Bitter Truth !!! .....Which Shouldn't Be Left To Continue And Remain That Way !!!
 


Watu Kila siku wanaamishwa kwa sababu mbali mbali za maendeleo iwe ujenzi wa miundombinu, maeneo ya jeshi, hifadhi nk

Hawa mayeroo watahama tu kwa hiyari au shurti kama wanajiona wao ni special sana watakipata wanachokitafuta.
 
Watu Kila siku wanaamishwa kwa sababu mbali mbali za maendeleo iwe ujenzi wa miundombinu, maeneo ya jeshi, hifadhi nk

Hawa mayeroo watahama tu kwa hiyari au shurti kama wanajiona wao ni special sana watakipata wanachokitafuta.
 
Back
Top Bottom