Must read: Elimu kwa watumiaji wa huduma za Mawasiliano/Simu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
TAHADHALI DHIDI YA UHALIFU NA UTAPELI UNAOFANYWA KUPITIA MITANDAO YA MAWASILIANO

_UNAPOTUMIA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO:_

```1. Unatakiwa kutumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa majina yako sahihi. Kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010, adhabu ya kutofanya hivyo ni faini ya shilingi 500,000 au kifungo miezi mitati (3). Kuthibitisha usajili wako, piga *106#.

2. Hakikisha taarifa unazotoa wakati wa usajili ni za kweli. Taarifa hizo zikiwa ni pamoja na mahala unapokaa, namba zengine za simu, nakala ya kitambulisho chako, nk. Adhabu ya kutofanya hivyo ni fainni ya shilingi 3,000,000 au kifungo miezi 12 au vyote kwa pamoja.

3. Kila mtumiaji wa simu ya mkononi anapaswa kuinakiri serial namba (IMEI) ya simu yake na kuihifadhi mapaha ambapo pindi akiitaka nje ya simu yake basi aweze kuipata na kuifanyia kazi inayotakiwa. IMEI ni kifupisho cha International Mobile Equipment Identifier. Ni namba pekee kwa kila simu ulimwenguni. Kujua IMEI yako, piga *#06#.

4. Ukipoteza simu au kadi ya simu (chipset) toa taarifa kwa mtoa huduma na Polisi. Adhabu ya kutofanya hivyo ni faini ya kati ya shilingi 300,000 na 500,000 au kifungo cha miezi sita (6) au vyote kwa pamoja.

5. Ukiokota simu au kadi ya simu toa taarifa polisi au kwa mtoa huduma. Adhabu kwa mujibu wa kifungu 126 ni shilingi 500,000 au kifungo cha miezi mitatu (3).

6. Epuka kununua simu mitaani/mikononi kwani huwezi jua simu hiyo iko salama kiasi gani. Nunua simu kwenye maduka yanayotambuliwa na upatiwe risiti halali inayotambulisha simu uliyonunua kwenye duka hilo.

7. Usitekeleza maagizo yoyote yanayohusu fedha kwa ujumbe wa maandishi hata kama yanatoka kwenye namba ya mtu unayemfahamu. Mpigie aliyekutumia ujumbe kwa simu nyingine uzungumze naye ili kuhakikisha kwamba ni yeye.

8. Ukipigiwa simu na mtu yeyote kuhusu masuala ya fedha, hata kama unadhani unamfahamu mtu huyo, mpigie tena kwa namba yake unayoijua.

9. Usitekeleze maagizo yoyote kutokana na ujumbe wa simu za mkononi unakutaka kutuma fedha kutoka namba ambayo mtumiaji wake unamfahamu na ambao unakueleza kwamba simu yake ina hitilafu hivyo hawezi kuongea, usitekeleze maagizo hayo.

10. Ukipata ujumbe kwamba umepokea fedha kwa njia ya simu, mpigie aliyekutumia na usitoe pesa hadi uthibitishe kwamba zimetumwa kwa nia njema.

11. Ikibidi kutuma pesa kwa mtu unayemdhani ndio muhusika, usikubali kutuma pesa kwenye namba ulizoambiwa utume hata kama atakwambia urahisi wake ni utume kwenye namba hizo anakwambie utume, wewe usikubali bali tuma pesa kwa namba za mtu huyo uliyemdhani ndie mhusika. Usitume pesa kwenye namba nyengine zaidi ya namba yake. Kama hana usajili wa mobile banking basi mwambie aje kuchukua mkononi mwako.

12. Iwapo unafanya biashara ya huduma za simu (mobile banking, salio la kurusha) hakikisha kwamba simu unayotumia kwa miamala ya kifedha ni tofauti na unayotumia kwa shughuli nyengine. Na hakikisha simu hiyo haitumiwi na mtu mwengine. Hivyo waagize wahudumu wako wasipokee maagizo ya mtu mwengine kuhusiana na biashara yako.

13. Tumia namba ya siri ambayo si rahisi mtu mwengine kukisia. Usitumie mwaka wako wa kuzaliwa au wa mtu wako wa karibu.

14. Thibitisha na hakiki namba ya mtu unayemtumia pesa au salio kabla ya kutuma.

15. Usimpe mtu yeyeto usiyemfahamu vizuri simu yako au kadi yako ya simu ili atumie.

16. Usitoe maelezo yoyote kuhusu namba yako ya simu au taarifa za binafsi kwa mtu yeyote anayekupigia simu hata kama atajitambulisha kuwa ni mtoa huduma kutaka taarifa hizo.

17. Epuka sana watu wanakupigia simu au kukutumia ujumbe kwamba kuna mradi ambao unalipa pesa nyingi na wanataka kukushirikisha. Hao ni matapeli. Jiulize kwa ulimwengu wa leo watu usiowajua wawezeja kukutajirisha wewe na wasiwatajirishe ndugu zao!

18. Epuka kuendelea na mazungumzo na watu wanaojitambulisha kuwa ni Majini kwani kwa hali ya kawaida jinni hawezi kumiliki simu na mitandao ya simu ikamsajilisha line, jinni akawa ananunua salio anaingiza kwenye simu yake na akakata mawimbi ya huduma za mawasiliano. Hao ni matapeli tu wanabadilisha sauti zao ili kukuteka akili uhisi unaongea na jinni.

19. Na inapotokea hali kama hiyo ya kupigiwa simu na mtu anaejitambulisha kuwa ni jinni unatakiwa haraka kujulisha kwa ndugu zako wa karibu, ili kama kuna element za ushirikina ziko ndani yake basi ndugu zako waweze kukuokoa kutotapeliwa.

20. Muda wote ukipokea simu, iwe simu ngeni au simu unayoijua (hali kadhali na SMS), jiweke kwanza kwenye hali ya usalama, kwa kujiweka mapema kwenye hali ya usalama unaweza kujua mapema nini kinaendelea kwenye mazungumzo hayo.

21. Ukifanyiwa uhalifu ambapo simu au mtandao umetumika kufanyia uhalifu huo toa taarifa Kituo chohote cha Polisi kilicho karibu yako.

22. Kwa tatizo ulilojulisha kwa mtoa huduma wako na ukakosa mashirikiano kutoka kwa mtoa huduma huyo, wasilisha malalamiko yako Mamlaka ya Mawasiliano ya Taifa (TCRA)```

*IMETAYARISHWA NA:*

```KITENGO CHA UCHUNGUZI WA MAKOSA YA MTANDAO
MAKAO MAKUU YA POLISI ZANZIBAR```
 
Thread kama hizi siku hizi humu ndani hazichangiwi ila weka thread ya Umbea au Ngono uone.
 
Somo murua. Naomba ikibidi mutoe vipeperushi vingi mgawe vijijini pia. Watu wengi wamelizwa sanaa kwa kutojua.
 
Back
Top Bottom