metatron
JF-Expert Member
- Sep 26, 2016
- 552
- 275
Kwanza kabisa wasalamu wanajumia hapa Jukwaani, baada ya kamaliza mfungo na Kisha sikuu ya Eid tunarejea kama kawaida.
Kwa vijana wa sasa ambao tumezaliwa Mkoani Mara katika wilaya ya Musoma Miaka ya 1980,1990. Kuna baadhi ya radha tulizipata kupitia mkoa wetu pendwa pamoja na matukio mengine ya kusitikitisha na kufurahisha kipindi hicho. Kwa kweli huwa nikikumbuka mpangangilio wa zile shule za msingi pale Musoma mjini huwa napata stajabu na kuwapa hongera waliofanya ubunifu ule.
1. Shule ya msingi Azimio
2. Shule ya msingi Mwembeni
3. Shule ya msingi Iringo
4. Shule ya msingi Mkendo.
Ukirudi katika viunga vya mji kwa wakati huo tuko wadogo Mida ya Jioni mitaa ya Iringo hapa kuna soko jioni unaenda kujipatia kichwa cha samaki sangara kwa Jina maarufu "Spika" Hahaha kwa kweli ilikuwa raha sana.
Kwa upande wa majina maarufu kipindi hicho MAMAS HOTEL, TAJIRI PANJU, SHARIFU (Sasa marehemu), KAKINDA, SULTAN (hapa walikuwa wanauza koni), JUMBA LA SINEMA, MILANGO MMOJA, KITAJI, CHAMBIRI, MSETI, MUSOMA BUS (na mengineyo utaweka unalokumbuka)
Sehemu za kutisha kipindi hicho ilikuwa ni makoko huko tuliambiwa kuna mtego wa Nyuki na huko ndio mafagio yalikuwa yanatoka. Habari mbaya nayokumbuka ilikuwa ni ajali ya Boti kuzama na iliua karibia watu wote waliokuwa wanaenda kuchukua Dagaa vizingani kama sikosei ilikuwa 1992 au 1993 maiti zikaletwa pale Mwigobole Mji mzima ulikuwa ni vilio tupu.
KAMA KUNA KITU UNAKUMBUKA UNAWEZA KUWEKA HAPA TUJIKUMBUSHE NA MUSOMA YETU.