PreGE2025 Musoma: REA yatoa elimu kwa wananchi kuhusu kutumia fursa ya miradi ya REA, wananchi waomba huduma hiyo ifike maeneo yote ambayo bado hajafikiwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Wananchi mkoani Mara wamesisitiza kuridhishwa na utekelezaji miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), inayotekelezwa nchini kwa lengo la kuwapatia umeme wa gharama nafuu.

Hayo yamejiri wakati Wataalam wa REA walipofika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutumia fursa ya miradi ya REA inayotekelezwa katika Kata ya Kwangwa wilaya ya Musoma mkoani Mara.

Awali Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka REA, Abdulrazack Mkomij ametoa elimu kwa umma kuhusu gharama za kuunganisha umeme, matumizi bora ya nishati, kuhamasisha kuunganisha umeme, tahadhari za umeme na elimu kuhusu utunzaji wa miundombinu ya umeme.

Naye, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Mara, Omary Gwillah, amesema kuwa REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme mkoani humo ili wananchi wafanye shughuli zao kwa tija.

Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Kwangwa, Bwiso Kinanda, ameishukuru Serikali kwa kupunguza gharama za uvutaji umeme. Amewataka wananchi kutumia fursa hiyo ya uvutaji wa umeme.

Vile vile, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kwangwa B, Maxmilian Kunju akizungumza kwa niaba ya wananchi ameiomba REA kuendelea kufikisha umeme kwenye maeneo mengine mkoani humo ili wananchi wa Musoma wapate nishati ya umeme.

Credit - Ngasa TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…