Muslim Hassanali asibezwe, amezichanga vizuri kuelekea 2020. Huyu hajanunuliwa bali amenunua!

Kwanza kabisa nimeambiwa Muslim ndiye aliyefadhili kila kitu kuanzia ukumbi wa mkutano, press yenyewena posho zote za waliohudhuria. Amefanya hivyo kwa kusudi maalum kabisa. Anaelewa anachokifanya.

Hassanali anaelekea CCM huku kukiwa na uhakika kuwa Zungu hatogombea tena ubunge 2020 baada ya kuhakikishiwa kuwa atakikalia kile kiti cha mhimili uliomezwa ambao kila kwenye press ya ikulu lazima awepo mwenye mhimili. Hivyo Zungu anaenda kustaafu kugombea jimbo la Ilala.

Muslim Hassanali anaingia moja kwa moja kuwa mmoja wa wadhamini wapya wa CCM yeye hana mawaa hivyo JPM atamkubali kutokana na fikra zilizojengeka.Pia Hassanali hahitaji siasa za kiuana harakati ambazo zipo Chadema kwa wengi wao. Hahitaji kupigana kufa na kupona eti kuhusu katiba mpya? for what? Hahitaji kujua kama nchi ina udikteta? Ili afanye nini? Yule kwanza hana cha kufia!

Sasa Hassanali anahitaji kuwekeza, anahitaji pesa ili aendelee kutamalaki Kariakoo. Hahitaji kuwa kama kina Lissu, Mnyika, Bony, Lema na wengine. Haina maana kwake. Shida yake siyo siasa. Hivyo Chadema hapamfai katu.

Kwanza ni mtu wa kupongeza kuweza kudumu Chadema kwa muda wote huo. Labda alitegemea kuwa 2015 mambo yangeenda sawa. Akapoteza, amepima siasa za serikali hii ya awamu ya tano akaona kukaa upinzani kutahitaji nguvu na msuli kwelikweli kupata jimbo kama mbunge. Ameona nguvu zinavyowagharimu kina Lema, kina Lissu. Ameona jinsi wanavyoteseka. Sasa yeye Hassanali mabadiliko ya kimfumo sijui katiba wala hayamsaidii maana hana cha kufia. Ni sawa na Rostam Aziz eti leo umwambie aingie Chadema apiganie katiba mpya? Si utasubiri hadi Yesu arudi?

Kwa kweli na kwa dhati kabisa kumuweka Muslim ndani ya Chadema kwa sasa ni kumuonea,mwacheni aende akasake maslahi! Huyu hajanunuliwa bali amenunua! Wapo ambao wakihama wala huhitaji kutumia nguvu kujua kama wamenunuliwa ila siyo huyu.

Nenda Hassanali nenda kasake fursa! Frustrations za siasa waachie wengine wapambane wewe siyo wa aina hiyo!
Umeandika vizuri sana. Aende!
 
Sasa huo uzi unajibu maswali yako yoteeee...Ila ule uzi wenye sauti ya Magufuli akijiita kufuli la kuyafunga majizi na mafisadi unaweza kuuweka humu? Kisha utuambie kwanini Mwakyembe alisema kuwa atamfunga Lowassa na akapewa hadi uwaziri wa sheria ili amfunge na akashindwa? Halafu uniambie leo imekuwaje lile kufuli likasifia tena lile jizi na lifisadi ambapo lile kufuli baada ya kupewa uwezo limeshindwa kulifunga lile jizi na lifisadi? Au tayari lilishapigwa funguo malaya!
 
Baada ya kutafakari sana, huyu ndiye nitakayemchagua kuwa rais wangu!

Back
Top Bottom