mashikolomageni
JF-Expert Member
- Jan 5, 2010
- 1,570
- 193
Mwandishi wa habari Cyprian Musiba amefunguka na kulaani matumizi makubwa ya Rushwa na maovu mengine kipitia ukuta wake wa sura kitabu.
Cyprian Majura Musiba
TANURU LA FIKRA
Sambala Nakushukuru..
Inasikitisha kuona Vijana wa sasa tena wengi wao watoto wa maskini kama mimi wanatetea Maovu..wanatetea wezi wa Maliasili za Tanzania,,wanatetea Vibaka wasiolipa kodi,,Wanatetea Majambazi yasiyotumia Slaa wala Risasi,,CCM ni chama cha watu,,CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi,,Uongozi ni Maisha ya watu,,hatuwezi kuhama CCM kwa kuwaogopa baadhi ya wezi na majangiri waliojificha CCM ili watekeleze wizi wao,,tutaendelea kubaki CCM na tutaendelea kusema hata tukiwa nje ya Uongozi,,chama hiki ni chama cha wakulima na wafanyakazi,,hatuwezi kuogopa kusema namna chama kinavyotafunwa na majambazi waliojificha kwenye CCM eti tutaambiwa tumeshindwa,la asha tutasema kila wakati na ikiwezekana hata kuandamana tukiwa tumevaa sare za CCM kupinga Mafisadi waondolewe katika chama hiki kilichotukuka afrika,na duniani,,Vijana wazalendo tuliomo ndani ya CCM tunapaswa kuungana kuwapinga wezi,,kupingwa rushwa,,na wale wanaotumia chama kujinufaisha huku wakiwaacha wananchi wanatahabika..haya siyo lazima yasemwe na Mbowe ama Lisu ndio yaonekane ya maana,,CCM itajengwa na kusimamiwa na wanaccm wenyewe..lazima tuwe na utaratibu wa kumsaidia kiongozi wetu wa nchi na mwenyekiti wa chama kupambana na haya majambazi haya yaliyojificha kwenye chama ili yatekeleze wizi na ujanja ujanja wao..
Naomba kuuliza kama mwanachama wa ccm anagombea tu UNEC wa Wilaya ama mwenyekiti wa CCM mkoa ama wilaya ama UWT ama wazazi anatumia zaidi ya milioni 300 kwa nafasi ambayo haina mshahara wala malipo,,unategemea huyu jamaa anaweza kuwatetea watanzania wanateswa na mfumko wa bei? huyu zaidi ataenda kutetea dili zake na wajanja wenzake ambao wamemsaidia kwa michango kumweka katika nafasi ya uenyekiti wa CCM wa Mkoa ama wilaya..kwa nini wafanyabiashara wote sasa wanakimbilia kwenye uongozi CCM hata wale wachafu kabisa wasiokuwa na sifa,,
Kwa kutumia fedha zao wanajaribu kushawishi wanachama wa ccm watenganishe Uenyekiti na urais,,wanawaza kutumia Fedha zao kumpandikiza mtu eti agombee uenyekiti wa ccm taifa,,hawa watu ni hatari kwenye chama ni tishio kwa mustakabala wa chama..
Kazi kwako ukinipiga ngumi ya sikio mimi napiga ngumi pua..