Musharraf arudi nyumbani pakistan

Musharraf arudi nyumbani pakistan

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,069
Reaction score
34,839
[h=1] Rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Musharraf, amerudi Pakistan, baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka minne.[/h]
130324115705_pervez_musharraf_return_karachi_304x171_afp_nocredit.jpg

Amepuuza vitisho vya kifo na kuamua kurudi nyumbani Pakistan
Musharraf amerudi nyumbani licha ya vitisho vya kifo mara kwa mara.
Wanajeshi maalum waliojihami kikamilifu walimpokea katika uwanja wa ndege wa Karachi, mara tu ndege hiyo ilipotua kutoka Dubai.
Mkutano mkubwa uliotazamiwa mjini Karachi kumlaki ulipigwa marufuku.
Jenerali Musharraf anatazamiwa kukiongoza chama chake katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei.

Huku hayo yakiendelea, wanajeshi 17 waliuawa katika shambulio la mtu aliyejilipua kwa mabomu katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Pakistan.
Walishambuliwa katika kizuizi cha kuwakagua watu kaskazini mwa Waziristan, karibu na mpaka wa Afghanistan.
Eneo hilo linafahamika kuwa ni ngome ya wapiganaji wa Taliban na vile vile wale wa al-Qaeda.
Ukanda wa video hivi majuzi ulielezea namna walenga shabaha watampiga risasi Jenerali Musharraf, au hata kumshambulia kwa watu watakaojitoa mhanga kwa kujilipua kwa mabomu.
chanzo BBC
 
Nimeona kapokelewa na special forces , anajindaa kwa uchaguzi wa mei ila hapo alipo anawindwa sana na maadui zake wakiwamo taliban sijui itakuwaje
 
Rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Musharraf, amerudi Pakistan, baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka minne.

130324115705_pervez_musharraf_return_karachi_304x171_afp_nocredit.jpg

Amepuuza vitisho vya kifo na kuamua kurudi nyumbani Pakistan
Musharraf amerudi nyumbani licha ya vitisho vya kifo mara kwa mara.
Wanajeshi maalum waliojihami kikamilifu walimpokea katika uwanja wa ndege wa Karachi, mara tu ndege hiyo ilipotua kutoka Dubai.
Mkutano mkubwa uliotazamiwa mjini Karachi kumlaki ulipigwa marufuku.
Jenerali Musharraf anatazamiwa kukiongoza chama chake katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei.

Huku hayo yakiendelea, wanajeshi 17 waliuawa katika shambulio la mtu aliyejilipua kwa mabomu katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Pakistan.
Walishambuliwa katika kizuizi cha kuwakagua watu kaskazini mwa Waziristan, karibu na mpaka wa Afghanistan.
Eneo hilo linafahamika kuwa ni ngome ya wapiganaji wa Taliban na vile vile wale wa al-Qaeda.
Ukanda wa video hivi majuzi ulielezea namna walenga shabaha watampiga risasi Jenerali Musharraf, au hata kumshambulia kwa watu watakaojitoa mhanga kwa kujilipua kwa mabomu.
chanzo BBC

halafu aliwahi kuwa kipenzi cha wakubwa wa magharibi huyu mzee
 
huyu mzee ana uchu wa madaraka, kwanza kaitawala pakistan kwa muda mrefu, kaua watu wengi kaiharibu nchi, kakoswakoswa kupinduliwa mara nyingi lakini bado hajaridhika.
Sidhani kama mara hii atasalimika si ajabu atalipuliwa kama alivyomlipua Benazir Bhutto..
 
Alipokuwa president alimzuia mwanasiasa nawaz sharif aliyetaka kurudi pakstani tokea exile saudi arabia na dubai alipokuwa akiishi...ndege iliyombeba nawaz shariff ilipotua pakistan alizuiwa kushuka na akaambiwa arudi alipotoka !!! Ila yeye musharaff ana support kubwa ya jeshi ata mkuu wa majeshi wa sasa aliteuliwa na yeye musharaff...akitafuta wanasiasa wazuri na kuwashawishi ku join anawezarudi madarakani as you know in politics anything is possible....wapakistani wengi niliozungumza nao wanampenda na wanasema hakuiba sana kama ma PM wengine...butto..nawaz shariff etc...alikuwa kipenzi cha magharibi kwa kuwa alipigana sana na taliban ndio maana taliban walitishia kumwua pindi atakaporudi pakistan...kumbuka pakistan ni nchi ngumu sana kuitawala so wanaitaji mtu kama huyu...ni ngumu sana kisiasa na ata wananchi wake..hiki chama kilichopo sasa madarakani ndio chama pekee ambacho kimechaguliwa na kinaenda maliza awamu yake...vingine vinaishia kupinduana tu
 
huyu mzee ana uchu wa madaraka, kwanza kaitawala pakistan kwa muda mrefu, kaua watu wengi kaiharibu nchi, kakoswakoswa kupinduliwa mara nyingi lakini bado hajaridhika.
Sidhani kama mara hii atasalimika si ajabu atalipuliwa kama alivyomlipua Benazir Bhutto..

Musharraf hawezi kusalimika Pakistan!
 
Back
Top Bottom