Steven mushi mushi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2016
- 533
- 739
Leo nilikuwa nafuatilia moja kati ya hotuba za rais wa Uganda Yoweri Museveni na katika hotuba hizo kuna sehemu anazungumzia tofauti ya maendeleo kati ya bara la Africa na mabara mengine na anasema kwamba tangia zamani wazungu wao waliamua kuchagua kazi na ndo maana maendeleo yao ni makubwa mno ukilinganisha na bara la Africa ambalo maendeleo yao yapo chini mno na ndo maana nchi nyingi za kiafrica licha ya kujitawala kwa zaidi ya miaka 60 bado tunaomba misaada ya vitu kama chakula na madawa kutoka Ulaya.
Na akaongeza kuwa ndo maana tajiri wa dunia bill gate ambaye utajiri wake ni zaidi ya dola za kimarekani billion 200 ana mtoto mmoja tu wa kike wakati utamkuta mwafrika ambaye ni maskini wa kutupwa ambaye hana hata ndururu ana watoto zaidi ya kumi na tano.
Pia rais huyo amezungumzia mfumo mbovu wa utawala wa Africa kuwa ndo chanzo kikubwa cha kutokukua kwa uchumi katika bara la Africa na kuongeza kuwa unakuta kiongozi wa Africa mfano rais ameshindwa kuleta maendeleo lakini anang'ang'ania madaraka badala ya kuachia wengine wenye uwezo wa kuendesha nchi na kuleta maendeleo na pia akawaasa viongozi wa Africa waaache uroho wa madaraka ambao wakati mwingine husababisha umwajikaji wa damu kwa raia wasio na hatia na kuwashauri kwamba kama umeandaliwa uchaguzi na kiongozi akashindwa basi ni sharti akubali matokea ili asibabishe vurugu na umwajikaji damu kwa raia wasio na hatia.