Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Hiyo ni kauli ya Rais Mteule wa Uganda, Yoweri Kaguta Meseveni alipokuwa akihojiana na mtangazaji wa BBC Swahili Zuhura Yunisi. Rais Museveni amedai kuwa wapinzani Afrika wanapenda kuendesha siasa kwa kuchanganya na uvurugaji wa amani jambo ambalo halipendezi na ndiyo maana Besigye anawekwa kizuizini.
Pamoja na hayo Rais Museveni ameulizwa ikiwa ana mpango wowote wa kufanya mabadiliko ya kikatiba kusudi kiti cha urais kiwe katika msimu wa kipindi fulani cha uongozi aidha miaka mitano au minne lakini Rais Museveni amegoma kuzungumzia jambo hilo akidai kuwa halina umuhimu kwa sasa.
Ushindi wa Rais Museveni umetiliwa shaka na baadhi ya waangalizi wa kimataifa akiwemo Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo aliyesema uchaguzi wa Uganda ulitawaliwa na usiri,ubabe na siasa chafu jambo linalotatiza uhalali wa uchaguzi huo.
Lakini pia katika anga za kimataifa, mgombea urais kupitia tiketi ya chama cha Republican anayeongoza katika kura za awali za maoni ameweka wazi msimamo wake dhidi ya wahafidhina barani Afrika hususani Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na Yoweri Museveni wa Uganda.
Naam, mwana JF nini maoni yako katika hili. Je, ni kweli kwamba wapinzani tu ndiyo hawajaiva kisiasa kwa kuwafananisha na wapinzania wa Ulaya au Marekani ama hata watawala wa Afrika hawajaiva kisiasa na kauli ya Museveni ni kuwapooza wafadhili wa Ulaya?