Museveni Na Ukame, Na Nionavyo...
Ndugu zangu,
Yoweri Museveni anasema, tishio la ukame kwa nchi za Maziwa Makuu ni ' Self inflicted'. Ana maana la kujitakia. Kaongea hayo akifungua Bunge la Afrika Mashariki.
Nimependa Yoweri Museveni alivyolichambua kisayansi zaidi jambo hili. Amezungumzia jinsi nchi zetu hizi zisivyosimamia vyema matumizi bora ya ardhi. Kwamba ujenzi na kilimo umeingia mpaka kwenye wetland, maeneo yowevu.
Kwamba vina vya maji vinapungua na mvua inatokana na mvuke unaotoka kwenye maji ardhini. Museveni analiona tishio la ukame kwenye Nchi zetu hizi za Maziwa Makuu. Naam, Yoweri Museveni ameongea kama Regional 'Stateman'- Kiongozi wa Kikanda.
Ukame na njaa ni vitu gani?
Nionavyo kwa nchi zetu hizi, na katika kuchanganya siasa hata kwenye masuala muhimu tumefika mahali kuna wenye kupiga mayowe kama ya yule mtoto mchungaji aliyekuwa akifanya utani wa kupiga mayowe ya " Jamani nimekutana na chui porini , jamani chui!"
Watu wazima kijijini wakatoka na silaha. Porini hawakukuta chui wala nyayo za chui.
Ikatokea mtoto yule siku moja akakutana na chui kiukweli akiwa machungani porini. Mayowe yake hayakusaidia. Watu wazima kijijini walimpuuzia.
Kisayansi njaa ni matokeo ya hali ya ukame. Kama nchi zetu hizi zitakaribisha vitendo vya mwanadamu vyenye kukaribisha ukame, basi, hakutakuwa na namna yeyote huko twendako ya kuepuka mabalaa ya njaa kwa watu wetu.
Tulipo sasa, hata kama tukikesha tunasali hilo pekee halitatosha kama hatutabadili matendo yetu kwa namna tunavyotumia ardhi ikiwamo uharibifu wa mazingira kwa kukata miti ovyo.
Ukilinganisha na wenzetu, Tanzania kama nchi tuna miundo mbinu mizuri ya kukabiliana na hatari za kimazingira zilizo mbele yetu.
Tuna nchi kubwa, ambayo, wakati kuna maeneo yenye kupata mvua haba, bado tuna maeneo mengi yenye mvua nyingi na mavuno ya kutosha na kujaza maghala kila msimu.
Tunahitaji kuweka miundo mbinu bora ili hata hao wenye kuzalisha kwa wingi wawe na hakika ya soko la bidhaa zao.
Tuna bahati pia ya kuwa nchi yetu ina amani ambayo ikitumika vema itaongeza uzalishaji na mavuno.
Tunahitaji kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima wetu juu ya matumizi sahihi ya ardhi na uhifadhi wa mazingira ili kuhakikisha uhakika wa mvua.
Mwisho, usalama wa chakula ni suala la kiusalama. Chakula kwa namna yeyote ile si suala la kulifanyia mzaha au siasa. Maana, kinapokosekana ndipo njaa hutamalaki.
Njaa ni Adui mkubwa na wa hatari kwa taifa lolote lile. Ndio maana wahenga walisema; Adui mwombee njaa.
Nchi haipaswi kuingia vitani kupambana na tishio la uvamizi wa adui njaa ikiwa na viongozi wake waliogawanyika. Viongozi wenye kutanguliza maslahi binafsi na ya vyama vyao kisiasa badala ya maslahi mapana ya taifa.
Maggid Mjengwa,
0754 678 252