Museveni: Bado sijaona kama Mwalimu Nyerere kwa sasa si tu Afrika bali hata kwa dunia nzima...ni wa Kipekee kabisa!

Viongozi wengi wa sadc na East Africa walikuwa vibaraka wa our great hero na Tz kwa ujumla
 
Tundu hana tofauti na wale watoto wa kambo mwanaume anayejitolea kulea mtoto wa mke wake kwa moyo mmoja, lakini kutwa kucha hilo toto Tundu ni kumtukana na kumkejeli baba mlezi huyo!
Bila kusahau wizi anaoufanya ndani ya nyumba ya baba mlezi akishirikiana na masela ya mtaani (Mabepari).
JK alikuwa kiboko, anapiga saini watu wa kazi wamshughulikie mtu pale mabwe pande halafu kesho asubuhi anakuwa wa kwanza kwenda kumpa mtu pole pale muhimbili.

Huyu mtu wa Singida anatembea na roho wa Mungu, vinginevyo sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine.
 
Vp nyerere alitawala kwa utawala bora mkuu?
Alifata mfumo wa kijamaa, na ujamaa uzaa udikteta, ujamaa na udikteta uzaa umasikini. Adui wa ujamaa na udikteta ni wasomi na matajiri, ujamaa utukuzwa fikra za MTU au chama, ubepari utukuzwa fikra za wengi,na palipo na wengi hakiiharibiki kitu.ndo Maana ubepari uendana na demokrasia na demokrasia uleta maendeleo, hakuna udikteta kwenye ubepari.
 
Pamoja na kushindwa kwa MWALIMU kwenye uchumi, Lkn alikuwa mzalendo wa kweli kwa haya mawili kuunganisha nchi kwa lugha ya kiswahili, na kutoruhusu ardhi imilikiwe binafsi ingekuwa hivo tusingepata hata pa kununua SHAMBA uweke kibanda
 
Kwa hili namwunga mkono Museveni. Mwalimu alitusaidia hata sisi ambao wazazi wetu walikuwa wanategemea "Vilepa" tukasoma kama watoto wa Mawaziri. Tukifunga shule tunarudi nyumbani masanduku yetu ya kichina yakiwa yamejaa Karanga, Tan Bond, Miche ya Sabuni za Mbuni na Rumi, Toilet paper bila kusahau "Warrant" ya kupandia mabasi ya Kamata na Railway.

Nikiona mtu anamlinganisha Nyerere na hawa viongozi wa sasa natamani nimsomee Itikafu!
 
Baada ya Kufungua Kituo Kipya ya Uongozi nchini Uganda kilichoitwa Julius Nyerere Leadership Centre Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema bado mpaka leo hii hajaona Kiongozi mwenye maono, makini, mwerevu na mzalendo wa kweli kama Hayati Baba wa Taifa Nyerere.

Mara baada ya Watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Makerere Kumkabidhi Rais Museveni Zawadi yao ndipo Museveni nae akapewa wasaa wa Kuhutubia ambapo kama kawaida yake wala hakuficha Mapenzi yake mema na ya Kutukuka kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

" Ni kweli Afrika na Duniani kumekuwepo Marais / Viongozi wengi ila nisiwe mwongo hadi hivi leo kila nikitaka kuwalinganisha hao wengine na Baba yangu na Mlezi wangu wa Kisiasa Mzee Nyerere bado nakosa kwani nadhani huyu Mtu ( Nyerere ) Mwenyezi Mungu alimuumba kwa Udongo wa peke yake ambao aliubariki sana kuliko Udongo mwingine ambao alitumia kuwaumbia Viongozi wengine ".

" Nimefurahi sana kuanzishwa kwa Kituo hiki na hasa hasa kwa Kukiita jina la Julius Nyerere kwa kuamini ya kwamba Wanasiasa wa Uganda, Afrika ya Mashariki, Afrika na hata duniani kwa ujumla watakitumia ili waweze kujifunza aina mbalimbali za Siasa na Uongozi kama Urithi wake mwenyewe Baba wa Siasa za Ukombozi barani Afrika Mzee Nyerere ".

Watanzania tufanye mambo yetu yote ila tukae tukijua ya kwamba Heshima yetu huko nje ya mipaka yetu inabebwa na itaendelea kubebwa sana na juhudi zake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hivyo nasi kama Watanzania yatupasa tujivunie na tumuenzi huyu Mzee kwa nguvu zetu zote kwani japo sasa ni miaka 19 tokea atutoke duniani ila matunda ya juhudi zake ndizo zinatufanya Watanzania wengi leo tutembee hivi Vifua mbele huku tukitiririka na kuserereka kwa amani na upendo tofauti na nchi zingine / mataifa mengine.

Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Hayati Baba wa Taifa na wenye ' akili / upeo ' tutamlilia na kumkumbuka daima. Na nichukue pia fursa hii adhimu kabisa kuwataka Viongozi wa ngazi zote nchini Tanzania kuwa najua hamna ubavu wa kuwa kama Nyerere ( japo akina Yericko wala Steve wanajitutumua lakini bado ) ila basi katika 100% ya matendo yake igeni basi hata 65% hadi 75% ili nanyi baadae Vizazi mbalimbali duniani vije kuwakumbukeni.

Nawasilisha.

Source: State House Uganda
Makerere University
Siyo Mseven tu, ata mimi bado napata shida kupata kiongozi wa kulinganisha na Nyerere..!

RIP my grandpa..!
 
Museveni hana jipya, angekuwa anaamini hayo angestaafu kwa heshima
 
Sawa Lakini Yeye Anashindwa Kufuata Nyayo Zake?
Unafiq Tu Hana Lolote
Unafiki kivipi kwani kakuambia yeye anampango wa kupita mapito ya Nyerere? Kakuambia dunia nzima hakuna kama Nyerere kwa maana na yeye pia akiwamo, Kwani ni lazima watu wote waongoze kama Nyerere?
Wee jamaa ungekuwa karibu ningekutandika stick za kutosha sana, Aal-llaaah!!!
 
kwahiyo wale wanaomfananisha jiwe/kichaa na nyerere wanafanya makosa
Jiwe na udhaifu wake wote ukimuuliza ni mwanasiasa gani ambaye anampenda ni lazima atamtaja Mwalimu Nyerere. Na jiwe anao uthubutu kama wa Mwalimu, akiongea siku zote kauli yake inakuwa na uzito.
 
Pale shetani anapomtukuza Mungu lakini haishi maisha matakatifu kama Mungu
 
Back
Top Bottom