- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu
Nimeona hii video ikimuonesha Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambaye pia ni mgombea wa wa Urais kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Janury 2026.
Nimeona hii video ikimuonesha Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambaye pia ni mgombea wa wa Urais kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Janury 2026.
- Tunachokijua
- Madai
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram ameshiriki kipande cha video kinachomuoensha Rais wa Uganda, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Urais wa nchi hiyo kuelekea uchaguzi unaotarajiwa ufanyika Januari, 2026 akimuonya mwandishi wa habari wa CNN akae mbali na uchaguzi wa nchi hiyo la sivyo atauona moto.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa video hiyo imehaririwa kwa teknolojia ya Akili Unde (AI).
Ufutailia kupitia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa video hiyo imehaririwa kwa kuongezewa sauti ambayo haikuwepo katika video halisi ambayo Museveni alikuwa akizungumza na chombo cha habari.
Video halisi ilichapishwa Novemba 6, 2023 na Chaneli ya Youtube yenye jina la UG files yenye kichwa " Hard talk: Germany Press asks Museveni tough questions | Wise response".
Katika video hiyo Museveni alianza kwa kuulizwa kwanini utawala wake unaonekana kuwa ni wa kiimla ingali hapo awali ulionekana ni kama utawala wake ulionekana kama ni ushujaa na ndipo Museveni akaanza kuelezea shida ni nini.
Hivyo video hiyo si ya mwaka 2025 kama inavyoonekana na badala yake ni ya mwaka 2023 ambapo pia Museveni hakuzungumza maneno hayo ya kumuonya Larry Madowo.