Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,849
- 11,302
Hivi sasa Tanzania inawalipa engineers kwenye consultancies kutoka nje ya nchi mishahara ya kati ya $10 000 hadi $20 000 ambapo kodi imesamehewa pamoja na magari ya kifahari na nyumba bure. Sasa kwa nini wasiweze kumlipa mzawa kiwango kama hicho na analipa kodi?
Hii danganya toto ya kila siku kwamba hatuna uwezo umepitwa na wakati, tungekuwa hatuna uwezo wa kulipa mishahara hiyo kusingekuwa na exparts wanaokuja Tanzania. Madaktari, wataalamu ambao wamebobea katika fani nyingi wapo nje kwa sababu hawawezi kulipwa vizuri nyumbani. Wataalamu wa madini wapo tele bongo lakini wanalipwa kiduchu na haya makampuni uchwara etc.
Hiyo mishahara inatokana na mikataba tunayoingia na hao tunaowaita wahisani. Hizo $10,000 hadi $ 20,000 (?) inakuwa katika hiyo misaada(?) tunayopewa. Kama ni consultant firm (Cowi, Howard Humphreys n.k) hiyo mishahara ni kutokana na mapato yao. George Ali akiamua kuwalipa wahandisi wake $10,000 nae tutamlaumu?
Hao madaktari walio nje si mishahara tu iliyowakimbiza. Hivi mnaamini kweli nchi ya Tanzania inaweza kuwalipa wataalam wake wote hizo Benjamin mnazoshupalia? Nchi ya watu milioni 35 na yenye kupata mapato yasiyozidi $billioni moja kwa mwaka kutokana na exports zake. Linganisha na kipato cha mauritius yenye watu milioni moja. Tusigombee ulaji tu. Tuangalie namna gani ya kuhakikisha kuwa tunatoka katika hili dimbwi la umasikini! Na hii ndio maana inabidi tuwe wakali pale tunapoona hata hiki kidogo kinachukuliwa na wajanja. Na sio kudai ati na sisi tugaiwe sehemu ya hicho kiduchu bila kuwaangalia walio nyuma yetu. Hatutafika mbali kwa mwendo huo.
Ya hao wataalamu wa madini siyajui, isipokuwa katika fani yeyote uzoefu unathaminiwa kama vile ambavyo elimu inathaminiwa. Kuwa na digrii peke yake haitoshi. Inabidi uthibitishe kuwa unaweza kweli kutumia elimu yako. Sasa hayo machimbo yameanza hivi karibuni, hao wataalamu wetu wamepata wapi uo utalaamu wa kwenye migodi?

Fundi mchundo said:Hiyo mishahara inatokana na mikataba tunayoingia na hao tunaowaita wahisani. Hizo $10,000 hadi $ 20,000 (?) inakuwa katika hiyo misaada(?) tunayopewa. Kama ni consultant firm (Cowi, Howard Humphreys n.k) hiyo mishahara ni kutokana na mapato yao. George Ali akiamua kuwalipa wahandisi wake $10,000 nae tutamlaumu?
Fundi mchundo said:Hao madaktari walio nje si mishahara tu iliyowakimbiza. Hivi mnaamini kweli nchi ya Tanzania inaweza kuwalipa wataalam wake wote hizo Benjamin mnazoshupalia? Nchi ya watu milioni 35 na yenye kupata mapato yasiyozidi $billioni moja kwa mwaka kutokana na exports zake. Linganisha na kipato cha mauritius yenye watu milioni moja. Tusigombee ulaji tu. Tuangalie namna gani ya kuhakikisha kuwa tunatoka katika hili dimbwi la umasikini! Na hii ndio maana inabidi tuwe wakali pale tunapoona hata hiki kidogo kinachukuliwa na wajanja. Na sio kudai ati na sisi tugaiwe sehemu ya hicho kiduchu bila kuwaangalia walio nyuma yetu. Hatutafika mbali kwa mwendo huo.
Fundi mchundo said:Ya hao wataalamu wa madini siyajui, isipokuwa katika fani yeyote uzoefu unathaminiwa kama vile ambavyo elimu inathaminiwa. Kuwa na digrii peke yake haitoshi. Inabidi uthibitishe kuwa unaweza kweli kutumia elimu yako. Sasa hayo machimbo yameanza hivi karibuni, hao wataalamu wetu wamepata wapi uo utalaamu wa kwenye migodi?
Chuo cha madini Dodoma hakifundishi utaalamu wa kuchimba madini. Wanafundisha utaalam wa kutafuta madini. Geology haimo kwenye Civil engineering, ni fani pekee.Wataalamu wa vitabu tuko wengi lakini nasisitiza kuwa utaalam wa nadharia nao ni muhimu. Hii kuheshimu mno makaratasi kwa upande ndio kumetufikisha hapa tulipo. Angalia wenye Ph.D na maprofesa wanavyohema katika kuongoza. Academics ni kitu kingine na uongozi kitu kingine.Hivi unaamini kwa nafsi yako kabisa hayo ni mapato yao? Kwa nini wasiende kufanya kazi huko kwao walipane bila kutupatia sisi longo longo. Tanzania tumekuwa conduit ya kunyonywa na hawa vibaka. Leo hii Japan akitoa msaada wa kujenga barabara anafahamu jinsi tusivyo na akili kwani tutanunua magari mikweche ambayo hana sababu ya kuwa nayo na ataweza kuingiza pesa nyingi kwa njia hiyo bila sisi wenyewe kujua nini kinaendelea. Hatuhitaji hii misaada ambayo inatafunwa na wenye meno makali, rejea import support pesa zilivyotafunwa BOT.
Sasa nadhani Mheshimiwa Duwa unakosea. Kampuni ya CowiCosult, Howard Humphrey ni kama kampuni yeyote inayofanya biashara.
apato yanatokana na kazi za ushauri wanazofanya. Kama Tan Consult na nyingizeyo. Hawa wote, wanalipana kutokana na kazi wanazozifanya. Sasa leo unataka tukawaingilie hata wanavyolipana? Na kwa taarifa yako humo humo wako watanzania ambao ni maboss. Makampuni mengine ya kigeni kama CarlBro, yalishindwa biashara wakafunga ofisi wakaondoka. Hao maengineer unaowazungumzia wanakuja kama technical support, ambao wanaunganishwa katika hiyo misaada tunayoomba. Dawa ni kutoomba misaada! tunaweza hilo? na ni busara?
Hizo pesa za import support si tulishirikiana kuzitafuna?
Sasa wewe unapenda jinsi WTZ wanavyokufa kama inzi pale Muhimbili wakati viongozi pekee ndio hawaishi kwenda kujipima kila mwaka kwa pesa ya walipa kodi? Gharama hiyo ni lazima ilipwe hakuna cha bure ndio sababu tunapiga kelele hapa kwamba tunaibiwa hadi rasilimali zetu kwa bei ya peremende. Hivi hujiulizi kwa nini mashangingi yamejaa TZ kuliko hata miji kama LA na sehemu nyinginezo? Ujinga umewatawala viongozi wetu kwa majibu mepesi ambayo yanahitaji majibu magumu. Huwezi kukwepa gharama ni lazima uongeze export au ufe uchaguzi ni wako. Tuachane na misaada na tuweze kuchangia bajeti yetu sisi wenyewe.
Nani aliesema mimi nafurahia kufa kwa wagonjwa wetu pale Muhimbili? Ninachokata ni majibu ya kirahisi kutoka kwenu ati tukiuza mashangangi dawa zitamiminika mahospitalini!Nakubaliana na wewe kuwa hizo rasilimali tunazoibiwa ni lazima tukemee kwa juhudi zetu zote. Haya niambie, wewe mtaalam, tutaongeza vipi hizo export? Kwa kuuza korosho?
Kwa taarifa yako WTZ wengi sana walisomea pale chuo cha madini Dodoma wakati wa enzi zile, hicho chuo kama sikosei kilijengwa na wajerumani (natumaini unaifahamu historia vizuri waliondoka lini) wengi wao wanafanya kazi nje ya Tanzania unaweza kuwapata Botswana, Norway, South Africa na nchi nyinginezo hata hivi sasa ukienda Bulyanhulu wapo wabongo wenye sifa kuliko hao wakubwa wao ambao waliletwa kuwa ndio wajuzi. WTZ hawakuacha kusoma geology ni mchepuo ambao uko kwenye Civil engineering (baadaye una-specialize) sasa hili la kusema tumeanza leo sijui linatoka wapi pengine wewe unafikiria kwa sababu madini yameuzwa kinyemela juzi juzi ndio tumeanza kusomesha. Mwalimu alisema ni bora tuyaache huko huko chini hadi wabongo wawe na akili lakini vibaka wameingia ni jukumu letu kuwasafisha.
Na hao wabunge wanaolipwa mishahara na marupurupu mazuri kwa kukutana kwa siku zisizozidi 90 kwa mwaka waliingia mktaba na nani? Je serikali haiwezi kuingia mkataba na wafanyakazi nao wakalipwa vizuri? Inakuwaje nchi kama Namibia, Botswana ziweze kuwalipa vizuri wataalamu wetu wakati Tanzania inashindwa kufanya hivyo!? Botswana na Namibia wametuzidi nini!?
Ni wapi nimesema hicho chuo kinafundisha utaalamu wa kuchimba madini?Chuo cha madini Dodoma hakifundishi utaalamu wa kuchimba madini. Wanafundisha utaalam wa kutafuta madini. Geology haimo kwenye Civil engineering, ni fani pekee.Wataalamu wa vitabu tuko wengi lakini nasisitiza kuwa utaalam wa nadharia nao ni muhimu. Hii kuheshimu mno makaratasi kwa upande ndio kumetufikisha hapa tulipo. Angalia wenye Ph.D na maprofesa wanavyohema katika kuongoza. Academics ni kitu kingine na uongozi kitu kingine.
Politics na longolongo kibao..
ingekuwa maendeleo ya nchi yanatokana na namna ya kujieleza basi wabongo tungekuwa dunia ya Kwanza!
Fundi Mchundo
Ni wapi nimesema hicho chuo kinafundisha utaalamu wa kuchimba madini?
Labda hufahamu geology inafundishwa kwenye Civil engineering kama somo pamoja na geotechnics na baada ya kumaliza ndio unafanya specialization. (muulize Civil engineer yoyote atakwambia) Siku hizi wameiweka kwenye kozi inayoitwa Earth Science and Engineering lakini ina uhusiano mkubwa na Civil Engineering kama huelewi hilo siwezi kueleza zaidi ya hapo.
....jidanganye tuu,this guy went to LSE then home tena serikalini kapangiwa planning officer mkoani,kilichotokea baada ya hapo God knows!
Kwa haraka haraka:
Human Development Index 2006:
Namibia 125
Botswana 131
Tanzania 162
Population
Namibia 2,009,000
Botswana 1,800,000
Tanzania 37,627,800
GDP
Namibia US$ 5.7 billion
BotswanaUS$ 9.0 billion
Tanzania US$ 10.9 billion
GDP/Capita (PPP US$) 2004
Namibia 7,418
Botswana 9,946
Tanzania 674
GDP/Capita (US $)
Namibia 2,843
Botswana 5,073
Tanzania 288
Under 5 Infant Mortality Rate per 1000 live births
Namibia 63
Botswana 84
Tanzania 126
Sasa bado unataka kujua wametuzidi nini? Tukubali umasikini wetu, tupambane nao ili tufike huko waliko wenzetu. Na hizi sio nchi zilizoendelea! Nenda kwenye site ya Human Development Report ya UNDP halafu linganisha nchi yako na vinchi kama Mauritius!
Hao wabunge ni sehemu ngapi ya watanzania 37 millioni? Nakubali kabisa kuwa mishahara wanayolipana ni aibu tupu na inastahili kukemewa! Lakini si kwa kusema na sisi tunataka hiyo hiyo! Tutawaua wenzetu.
Sasa na nyie watu, kama wote tunasema hatutaki kwenda kuwa planning officer kisa tumesoma LSE, nani ataendeleza hiyo nchi? Halafu sisi hatutaki hizo kazi, wakishika nafasi vilaza wanavurunda tunaanza kulalamika tena wakati sisi hatutaki kufanya hizo kazi! Hivi, haya maisha tunayoyafaida ya wazungu inabidi tujue kwamba kuna watu waliyahangaikia kipindi fulani, hayakushushwa mbinguni! Tunawajibika kuboresha maisha home ili vizazi vijavyo vije vifaidi kama sisi tunavyofaidi huku kwa wazungu. Tatizo letu wabongo/wafrika, tunataka tupande na kuvuna sasa hivi, katika hali ya kawaida haiwezekani!
Fundi Mchundo
Nafikiri una haja ya kuangalia ninachoandika bila kukurupuka. Nimekuuliza 'ni wapi niliposema chuo cha Dodoma kinafundisha utaalamu wa kuchimba madini? Hukuja na jibu na sasa unakuja na ngonjera nyingine kwamba nawalaumu wenye migodi kwa kutowaajiri, wapi hapo unaweza kunionyesha?
Sasa kama wewe ni Civil Engineer ilikuwaje ukasema 'Geology haimo kwenye Civil engineering?' Hivi kama hufahamu swali ni bora kuuliza kuliko kukurupuka. Huwezi kuwa Geologist bila kuelewa Geophysics na core geology foundation.
Mwenyewe unakiri hapo juu kwamba wanasoma as a basic sasa kama halina umuhimu kwa nini walisome? Unakula matapishi yako sasa.
Hivi unaamini kwa nafsi yako kabisa hayo ni mapato yao? Kwa nini wasiende kufanya kazi huko kwao walipane bila kutupatia sisi longo longo. Tanzania tumekuwa conduit ya kunyonywa na hawa vibaka. Leo hii Japan akitoa msaada wa kujenga barabara anafahamu jinsi tusivyo na akili kwani tutanunua magari mikweche ambayo hana sababu ya kuwa nayo na ataweza kuingiza pesa nyingi kwa njia hiyo bila sisi wenyewe kujua nini kinaendelea. Hatuhitaji hii misaada ambayo inatafunwa na wenye meno makali, rejea import support pesa zilivyotafunwa BOT.
Sasa wewe unapenda jinsi WTZ wanavyokufa kama inzi pale Muhimbili wakati viongozi pekee ndio hawaishi kwenda kujipima kila mwaka kwa pesa ya walipa kodi? Gharama hiyo ni lazima ilipwe hakuna cha bure ndio sababu tunapiga kelele hapa kwamba tunaibiwa hadi rasilimali zetu kwa bei ya peremende. Hivi hujiulizi kwa nini mashangingi yamejaa TZ kuliko hata miji kama LA na sehemu nyinginezo? Ujinga umewatawala viongozi wetu kwa majibu mepesi ambayo yanahitaji majibu magumu. Huwezi kukwepa gharama ni lazima uongeze export au ufe uchaguzi ni wako. Tuachane na misaada na tuweze kuchangia bajeti yetu sisi wenyewe.
Kwa taarifa yako WTZ wengi sana walisomea pale chuo cha madini Dodoma wakati wa enzi zile, hicho chuo kama sikosei kilijengwa na wajerumani (natumaini unaifahamu historia vizuri waliondoka lini) wengi wao wanafanya kazi nje ya Tanzania unaweza kuwapata Botswana, Norway, South Africa na nchi nyinginezo hata hivi sasa ukienda Bulyanhulu wapo wabongo wenye sifa kuliko hao wakubwa wao ambao waliletwa kuwa ndio wajuzi. WTZ hawakuacha kusoma geology ni mchepuo ambao uko kwenye Civil engineering (baadaye una-specialize) sasa hili la kusema tumeanza leo sijui linatoka wapi pengine wewe unafikiria kwa sababu madini yameuzwa kinyemela juzi juzi ndio tumeanza kusomesha. Mwalimu alisema ni bora tuyaache huko huko chini hadi wabongo wawe na akili lakini vibaka wameingia ni jukumu letu kuwasafisha.
Usituletee longolongo lako hapa. Tanzania ina uwezo kabisa wa kulipa mishahara mizuri kwa wafanyakazi wake ili waweze kumudu gharama za maisha. Kuna savings chungu nzima ambazo zinaweza kufanywa ili kupunguza gharama za uendeshaji wa siri kali. Kwa mfano wanaostahili kuwa na magari ya siri kali ni watu wachache sana kama vile Rais, Waziri Mkuu labda na spika wabunge wengine wote wawe na magari yao binafsi na gharama za uendeshaji ziwe juu yao wenyewe. Hapa tutapunguza gharama chungu nzima. Mikataba kama ikiandikwa kwa kuwekwa mbele maslahi ya Taifa basi mapato ya Taifa yataongezeka kwa kiasi kikubwa sana haya pia yanaweza kuhakikisha ulipwaji wa mishahara mizuri kwa Watanzania.
Wimbo wako wa 'Tanzania nchi maskini umeshapitwa' na wakati ulikuwa unaimbwa mwaka 47 lakini sasa hivi haukubaliki tena. Tuna rasilimali chungu nzima ambazo kama zikitumiwa vizuri pamoja na kuwa na population ya 39 million, tunaweza kabisa kuhakikisha maisha mazuri kwa kila Mtanzania. Lakini viongozi wamekuwa mafisadi, wizi, wanaopenda kujitajirisha kupitia nyadhifa zao. Leo hii kuna tofauti kubwa sana kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho. Inakuwaje watu wengine wana maisha kama ya wacheza sinema wa Hollywood wakati huo huo mamilioni ya Watanzania hawajui hata mlo wao mwingine wataupata wapi!?
Wewe kama unataka kuishi kwa shida basi ni wewe pekee yako, Watanzania wote na wao wanataka waone matunda ya elimu yao na kuajiriwa kwao kwa kulipwa mishahara inayoendana na gharama halisi za maisha siyo kuwalalia. Hakuna Mtanzania yeyote atakayekufa kwa kuwa na mishahara na marupurupu mazuri, labda utakufa wewe usiyetaka mshahara wa kufuru. Usipende kujishushia hadhi kaka (mie mshahara huu mkubwa sana, sistahili kuupata) 😕 , ukijidharau mwenyewe hapa duniani basi kila mtu atakudharau.