Muono wa muoaji

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,792
Kojo alikwenda masomoni Ughaibuni kwa miaka mitano, alihitimu kama mhandisi, baada ya kurudi nyumbani aliajiriwa na taasisi ya umma. Baada ya miaka mitano vijana wengi aliowaacha nyumbani walikuwa wameshaoa na kuolewa, alitamani sana kupata mwenza wa kuanza nae maisha.

Kojo alikutana na dada No1 huyu dada aliitamani sana ndoa, alikuwa anasubiri siku Kojo atakapotamka neno hilo. Kojo alikuwa mcha Mungu sana, na kila kitu kinacho husu maisha yake hakukifanyia papara. Dada No1. alianza kumuuliza Kojo kama anampango wa kuoa katika maisha yake, Kojo alijibu bado hicho kitu sijakiwaza. Mwaka ulikatika wakiwa kwenye mahusiano, dada No1 siku isiyo najina alimpigia simu Kojo akamwambia kuna mtu ameleta barua ya posa kwao, Kojo alimjibu na wewe unalionaje swala hili? Dada No1 alijibu kama wewe si muoaji usinipotezee muda, basi Kojo akamwambia midhali muoaji amekuja wewe endelea. Halikuwa jibu alilotegemea dada No1. Alianza kupiga simu kumuomba Kojo waongee, Kojo alimwambia tafadhali endelea na maandalizi ya harusi, na mimi niache nipange maisha yangu.

Sikujua kilichoendelea kwa dada No1. lakini huu ulikuwa mwisho wa uhusiano wao na Kojo. Kijana Kojo akaendelea na safari ya kutafuta mwenza, rafiki yake wa karibu sana akawa anamueleza jinsi shangazi yake alivyoachika kwa mume na ameweza kulea mabinti wanne mjini kama single mother. Kojo aliuliza katika hao mabinti sasa hivi wana umri gani, basi rafiki bila kujua kuwa ana madini mkononi na amepata mteja, akamueleza juu ya ile familia. Kojo aliomba sana wamtembelee shangazi siku moja.

Rafiki alimtaarifu shangazi kuwa ninakuja na rafiki yangu J'mosi, shangazi mwenyewe anajibana na mabinti zake kwenye vyumba viwili, shangazi ameajiriwa kama mhudumu kwenye chuo hapa mjini, wale mabinti wawili wamemaliza shule na wamepata kazi mmoja yuko chuo na wamwisho bado anasoma secondary.

J'mosi ilipofika dada mkubwa alikuwa kibaruani, wapili na watatu ndio walikuwa nyumbani wa mwisho alikuwa tuition. Shangazi aliandaa maandalizi aliyoweza, wageni walifika, basi baada ya salamu wakaulizana habari, binti wa pili wa shangazi kujua jamaa ni mhandisi, tena bado yupo yupo, akaanza kurap, akawa anamueleza sehemu za starehe zilizopo mjini kama ameshazitembelea, Kojo alikuwa anasikiliza, akaja binti wa tatu wa shangazi, akawa yeye anamuuliza uwezekano wa kupata kazi katika shirika taasisi anayofanyia Kojo, maongezi yakaendelea.

Baada ya muda mrefu, alirudi binti wa kwanza wa shangazi kutoka kibaruani, baada kuwasalimia wageni, alikaa kimya akawa anasikiliza maongezi. Kojo alivutiwa sana na ukimya wa yule dada, sasa Kojo ndiyo akaanza kumuuliza unafanyia kazi wapi, ulisoma wapi? Baada ya pale J3 Kojo alimptembelea ofisini, na urafiki ulizaa ndoa.
 
Hii inaitwa ~be first to reply~

Turudi kwenye Maada. Mada ni nzuri Ila nasikitika sana kusema kwamba "Mwalimu wa akina Dada asilimia 90, alishafariki, mbali na kufariki alikuwa kipofu na kiziwi"

Kwa misingi hiyo, wadada wengi wamecopy kutoka kwa mwalimu wao vitu wasivyovijua sana..

Heri yake Dada wa kwanza ambaye yuko kwenye 10% ya Dada wote welevu duniani. But 90% ni manungayembe..
 
Hii inaitwa ~be first to reply~

Turudi kwenye Maada. Mada ni nzuri Ila nasikitika sana kusema kwamba "Mwalimu wa akina Dada asilimia 90, alishafariki, mbali na kufariki alikuwa kipofu na kiziwi"

Kwa misingi hiyo, wadada wengi wamecopy kutoka kwa mwalimu wao vitu wasivyovijua sana..

Heri yake Dada wa kwanza ambaye yuko kwenye 10% ya Dada wote welevu duniani. But 90% ni manungayembe..
Dada wa kwanza alitingisha kibiri kilichojaa.
 
Nadhani nimeielewa, ila upande wangu nimeielewa tofauti kdgo " MUHUSIKA MKUU ANAWEZA KUWA HUKU!!?"
 
Back
Top Bottom