Muonekano wa sayari ya Saturn ukiwa na baadhi ya Miezi yake kadhaa

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Muonekano wa sayari ya Saturn ukiwa na baadhi ya Miezi yake kadhaa ikionekana kwa pamoja baada ya kuchukuliwa picha na mwanaanga chipukizi anayeitwa Danborjaa akiwa na darubini yake huko katika makazi yake.

Basi kama umeshazoea kuona Dunia yetu ikiwa na mwezi wake mmoja unastahajabu ya sayari ya Saturn ambayo yenyewe ina kiasi cha jumla ya miezi 83 inayozunguka sayari hiyo muda wote.

Tunafahamu kuwa ili gimba liweze kukam ata gimba lengine dogo dogo basi ni lazima kani ya uvutano wa gimba fulani iwe kubwa kuzidi ile ya gimba fulani mfano Dunia imeweza kukamata mwezi wetu kwakuwa gimba Dunia lina kani kubwa ya uvutano kuliko mwezi wetu basi ndio maana mwezi umekuwa ukimilikiwa na Dunia muda wote.

Saturn ni moja ya sayari yenye kiasi cha kani kubwa ya uvutano ndio maana imeweza kuvuta baadhi ya magimba mengi madogo madogo ambayo kwa namna moja ama nyengine ndio tunayoyaita miezi hayo magimba yaliyokuwa katika umiliki wa sayari hiyo Saturn.

Kama kutakuwa na gimba lengine lolote lile litakalokuwa linazagaa zagaa karibu zaidi ya eneo ambalo kuna kani kubwa ya sayari Saturn basi ni moja kwa moja litavutwa na kuwa katika mfumo wa umiliki wa sayari hiyo.

mzawa
Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili
FB_IMG_1674506333471.jpg
 
Mkuu, hiyo ring inayoizunguka sayari ya Saturn ni nini hasa?! Is it a tangible object or just a light?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sayari ya saturn imezungukwa na ringi ama pete zenye mabillion ya vipande vya barafu, mawe na vumbi zito ambavyo vilitokana na kuvunjika kwa miezi midogomidogo iliyokuwa kwenye sayari hiyo pamoja na comets na asteroids ambazo hazikuifikia sayari hiyo.
Mazingira ya sayari ya saturn ni ya baridi kali sana ambapo joto hushuka mpaka kufikia nyuzi -170 °C (kumbuka maji yanaganda kwenye nyuzi 0°C)
 
Mhuuuh, so interesting! Lakini kwa nini iwe kwa Saturn peke yake na sio sayari nyinginezo; zenyewe hazikuwa na atmosphere yenye comets, asteroids na mawe mengine vilivyogongana kuleta vipande vidogo vidogo na kusababisha muunganiko wa pete kama ya Saturn?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhuuuh, so interesting! Lakini kwa nini iwe kwa Saturn peke yake na sio sayari nyinginezo; zenyewe hazikuwa na atmosphere yenye comets, asteroids na mawe mengine vilivyogongana kuleta vipande vidogo vidogo na kusababisha muunganiko wa pete kama ya Saturn?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila sayari ni Tabia zake na jinsi inavyojiendesha thus why hakuna mfanano wa sayari zote kitabia

Labda kam itagundulika uko mbeleni
 
"We will show them Our signs in the universe and within themselves until it becomes clear to them that this ˹Quran˺ is the truth. Is it not enough that your Lord is a Witness over all things?"
41:54 qur an
 
Sii Saturn pekee ambayo ni sayari yenye rings ila hivo rings za Saturn ni kubwa kushinda rings za sayari nyinginezo. Jupiter, Saturn, Uranus na Neptune pia zina hizo rings ingawa hazionekani vizuri.
 
Attachments

  • jupiter rings.jpg
    jupiter rings.jpg
    3.2 KB · Views: 8

Similar Discussions

Back
Top Bottom